March 21, 2025 02:48:31 AM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

 
                               George H.W Bush.

ALIYEKUWA Rais wa 41 wa Marekani, George H.W Bush amekimbizwa katika hospitali ya Houston Methodist nchini Marekani baada ya kupatwa na tatizo la kupumua.

Alipelekwa katika hospitali hiyo kwa gari la kubebea wagonjwa (Ambulance) jana usiku.

Wawakilishi wa Bush wanasema kuwa hatua hiyo ya kupelekwa hospitali ni kama tahadhari.

Bush mwenye umri wa miaka 90 alikuwa madarakani tangu mwaka 1989-1993 na ndiye Rais mzee kuwahi kuiongoza Marekani akimshinda Jimmy Carter kwa miezi michache.

Alihudumu kwa muhula mmoja baada ya kushindwa na Rais Bill Clinton.

Bush ambaye hawezi kutumia miguu yake, hivi karibuni alionekana amekaa katika kiti cha magurudumo kwenye hafla iliofanyika mwezi Novembea katika chuo Kikuu cha Texas na mwanaye aliyekuwa Rais wa 43 wa Marekani, George W Bush.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
24 Dec 2014

Post a Comment

 
Top