March 17, 2025 10:32:13 PM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
141218151909_mbmw_carLakini hivi karibuni hautahihajika kupanda gorofa kutafuta gari lako kwani kampuni ya kutengeza magari ya BMW, imetangaza kuzindia kifuaa ambacho kinaweza kuyawezesha magari ya kampuni hio kujiegesha yenyewe kwa kubonyeza tu kifaa hicho.
Hata hivyo dereva wa gari hilo atalazimika kuvaa saa ya Smartphone mkononi ambayo ataibonyeza na kuiamrisha kwa sauti gari hilo kwenda kujiegesha.
Gari hilo kwa amri ya dereva litatoka liliko baada ya dereva kushuka na kwenda lenyewe kwa kuhesabu muda utakalichukua kwenda kutafuta sehemu ya kujiegesha.
Tawi la kampuni ya BMW mjini Munich, Ujerumani limezindua teknolojia hio ambayo inawezesha gari kujiegesha lenyewe.
Gari hilo linatumia miale ya Leser iliyo kujitafutia ramani ya jengo ambalo lipo. Dereva anaweza kuliamrisha gari hilo kwenda kujiegesha kwa kutumia Smartphone.
Teknolojia hio inajulikana kama ‘ Remote Valet Parking Assistant,’ na inafanyiwa majaribio kwenye gari la BMW i3.Badala ya kutumia GPS, teknolojia hio inatumia miale ya Laser ambayo hutengeza ramani inayolisaidia gari hilo kutafuta sehemu ya kwenda kujiegesha.
Teknolojia hiyo inaiwezesha gari hilo kuona njia na nafasi ya kujiegeshea na pia kuona vizingiti mfano kama magari ambayo hayajaegeshwa vyema.
Kwa mujibi wa waliotengeza gari hilo, linaweza kujitafutia nafasi ya kujiegesha na hata kuweza kutambua sehemu ambako kuna nafasi.
Teknolojia hio inatengezwa sambamba na teknolojia nyinginezo zitakazoweza kuzuia gari hilo kugongana na magari mangeine.
Tazama piccha ziko hapa chini
141218151840_bmw_car141218151909_mbmw_car141218151909_bmw_watch

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
24 Dec 2014

Post a Comment

 
Top