KASHFA ya uchotwaji wa zaidi ya Sh bilioni 300 kwenye akaunti ya Tegeta Escrow, imewachafua viongozi watatu ambao walishaanza harakati za kuusaka urais kwa mwaka 2015.
Baadhi
ya viongozi hao ni pamoja na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Mbunge wa
Sengerema, William Ngeleja na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, Profesa Anna Tibaijuka.
Kwa
upande wa Pinda, ripoti ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC)
iliyowasilishwa bungeni, ilionyesha kiongozi huyo wa shughuli za
Serikali bungeni alilidanganya Bunge kwa matamshi yake.
Mara kadhaa Pinda alisikika akiueleza umma kuwa fedha hizo hazikuwa za umma bali mali ya Kampuni ya Kuzalisha Umeme ya IPTL.
Katika
maazimio ya PAC, Pinda alitakiwa pia kuwajibika kutokana na kushindwa
kusimamia Serikali kwani katika hatua zote za kutolewa kwa fedha hizo,
alikuwa akijulishwa.
Pinda
ambaye alitangaza kuanza harakati za urais kimya kimya, akiwa jijini
London, Uingereza alipohojiwa na Kituo cha Televisheni cha BBC,
alijikuta kwenye wakati mgumu pale Bunge lilipopitisha azimio la
kumpeleka kwa mamlaka ya uteuzi kabla baadae jina lake kuondolewa.
Hali
hiyo ilijitokeza pale Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe alipolishauri
Bunge kupeleka majina ya watu wote waliotakiwa kuchukuliwa hatua kwa
mamlaka zao za uteuzi ili hatua zaidi zichukuliwe.
Baada
ya kauli hiyo ya Zitto, Spika wa Bunge Anne Makinda alilihoji Bunge na
kwa sauti moja likakubali kabla ya Mbunge wa Simanjiro, Ole Sendeka
kusimama na kuomba mwongozo wa Spika ambaye baadaye alitengua uamuzi
wake.
Akizungumza
na Mtanzania, Zitto alisema jina la Pinda kupelekwa kwa rais ingetosha
kuonyesha Bunge halina imani naye, hivyo mamlaka yake hiyo ya uteuzi
ingebidi itengue nafasi ya kiongozi huyo wa shughuli za Serikali
bungeni.
Alisema
pia kamati yake ilikubali kuondoa jina la Pinda kwenye orodha ya vigogo
waliopaswa kushughulikiwa baada ya mazungumzo kati ya wabunge wa
upinzani na wale wa CCM.
Kutokana
na hali hiyo, Pinda ambaye anajulikana zaidi kama ‘mtoto wa mkulima’,
harakati zake za kwenda Ikulu zimetiwa doa kwani mwanzo alihesabika kuwa
ni kati ya wagombea wasio na kashfa.
Kwa
upande wake, Ngeleja ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini,
anadaiwa kupewa Sh milioni 40.4 kutoka kwenye akaunti ya Escrow huku
Profesa Tibaijuka ambaye ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, akidaiwa kupewa Sh bilioni 1.6.
Viongozi
wote hao wawili ambao hawajawahi kutangaza rasmi kuwania urais mbali na
majina yao kutajwa kwenye orodha hiyo, Bunge limeazimia wachukuliwe
hatua.
Kwa
upande wa Profesa Tibaijuka, rais ametakiwa kumvua wadhifa wa uwaziri
huku Ngeleja ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba,
Sheria na Utawala, spika akishauriwa kumchukulia hatua ya kumvua wadhifa
huo.
Akichangia
bungeni, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu, Steven
Wasira, aliwataka wote wanaotumia suala la ripoti ya PAC kwa vigezo vya
kuwaondoa wenzao katika mbio za urais hawastahili kupewa nafasi hiyo.
“Wanaotaka
urais kama wapo ni pamoja na mimi, ambao wanaona mbinu ni kuwaondoa
wengine kwa nguvu, hao hawafai kupewa urais wa nchi hii. Urais ni lazima
ushindaniwe kwa haki na vyama vyote vipewe nafasi ya kushiriki. Kama
unataka urais ushindani uwe kwa njia sahihi,” alisema.
Alisema
ni bora kuwa maskini anayeheshimika kuliko kukubali kuwa tajiri
anayedharauliwa na kutukanwa kutokana na mapato yasiyokuwa halali.
Wasira
alieleza kwa kuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru)
imesema baadhi ya watu walikwenda kuchukua fedha wakiwa na magunia,
mifuko ya sandarusi, rumbesa na maboksi katika moja ya benki, ni vyema
uchunguzi ukifanyika ili kuwatambua watu hao na hatua zaidi zichukuliwe.
“Ni
lazima tufuatilie na vyombo vyetu vya sheria vituambie ni kina nani
hao, vinginevyo hatuna nchi. Tukubali hawa watu wabebe mizigo yao,
hakuna CCM ya wezi, ila kuna wezi ndani ya CCM, hivyo wezi ni lazima
wabebe mizigo yao,” alisema.
Alisisitiza
kwamba ripoti hiyo ya PAC inatakiwa kuheshimiwa na kwamba hakuna mtu
mwenye mamlaka ya kuihoji uhalali wake kwa kuwa inatokana na kamati
maalumu inayotambuliwa na Bunge iliyokusanya taarifa kutoka kwa vyombo
vinavyoaminika vya Serikali, ambavyo ni Takukuru na CAG.
Credit:Mtanzania
Credit:Mtanzania
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment