KWAKO mshindi wetu wa Shindano la Big Brother Hotshots 2014, Idris Sultan. Natumaini ndiyo kwanza una ‘kiraruraru’ cha ushindi wa milioni 510, hongera kwa ushindi!Mkwanja huo ni mrefu, hayo ni mafanikio yako binafsi lakini pia watanzania kwa jumla. Walikupigia kura, kweli umeshinda!
Ukitaka kujua hali yangu mimi mwananchi wa kawaida niko poa, naendelea na majukumu yangu ya kila siku na huu ndiyo uwanja wangu wa kujidai kama ulikuwa hauujui.
Madhumuni ya kukuandikia barua hii kwanza kabisa ni kukupongeza kama nilivyoanza hapo juu. Juhudi zako binafsi ndizo ambazo zilikuongezea nguvu ya kuendelea kubaki ndani ya mjengo achilia mbali zile kura za wananchi.
Jumba lile halina ‘formula’ za kukaririka. Kila mwaka Big anakuwa na vigezo vyake vipya hivyo inahitaji maono ya ziada kujua unatakiwa kufanya nini na kwa wakati gani, ili uweze ‘kumuwini’ Big, hongera maana ulimkalisha!
Pongezi hizo pia unapaswa kuzirudisha kwa Watanzania, uwashukuru kwa sababu angalau mwaka huu wameonesha kwamba wanaweza kupiga kura, miaka ya nyuma hali haikuwa hivi. Washiriki walikuwa wanajijua wenyewe, zaidi walipigiwa kura na mataifa mengine.
Hii iwe funzo kwa mashabiki ‘maandazi’, tunapaswa kuwapigia kura washiriki wetu pindi tunapopewa taarifa kuwa wanatuwakilisha katika mashindano yoyote kimataifa.
Weka hayo kando, nirudi katika suala lingine ambalo naamini huu ndiyo wakati muafaka kukwambia. Suala hilo ni namna ya kuzitumia fedha hizo ambazo mara nyingi watu wengi wamekuwa wakifeli.
Fedha nyingi ambazo hukuzichanga mdogomdogo na kukujia ghafla huwa ni rahisi sana kuyeyuka.
Zinayeyuka maana huwa wengi huponzwa na kale kakauli ka “bado zipo, ngoja ninyofoe kidogo. Nitaanzisha biashara baadaye kidogo.”Mifano ipo mingi, tazama kilichomtokea Richard Dyle Bezuidenhout aliyeibuka kidedea katika mashindano hayohayo mwaka 2011. Siwezi kumsemea sana lakini kimsingi licha ya kutapatapa katika kuziwekeza fedha hizo lakini hadi sasa mambo si mambo!
Ukirudi nyumbani, kuna washindi wa Shindano la Bongo Star Search, wengi wameishia kudondokea pua. Wameshindwa kuendeleza matunda ya ghafla wanayoyapata katika mashindano hayo.Wewe ndiyo kwanza umeshinda, kwanza tafakari kwa kina kabla ya kuanza kuzitumia hakikisha umefanya utafiti wa kutosha juu ya kitu husika, je kitakulipa? Washauri pia unapaswa kuwachuja tena ikiwezekana zaidi amini akili yako kuliko akili za kuambiwa.
Nikutakie matumizi mazuri ya mkwanja wako!
Wasalam,Erick Evarist.

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro

Post a Comment
Post a Comment