Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

MSANII nyota wa filamu Tanzania, Tamrina Poshi maarufu kama Amanda, amenaswa katika picha akiwa na mzungu anayeonekana kumzidi umri ambaye unaweza kumwita kijeba aliyemtambulisha kama rafiki yake.



 
Msanii nyota wa filamu Tanzania, Tamrina Poshi maarufu kama Amanda akiwa na mzungu.

Habari kutoka chanzo cha kuaminika zinasema, picha hizo ziliibwa katika simu ya msanii huyo na mtu asiyefahamika, ambaye kwa lengo lisiloeleweka, alianza kuzitawanya kwa watu mbalimbali.


Inadaiwa kuwa Amanda amekuwa akionekana sehemu tofautitofauti jijini Dar akiwa na mzungu huyo ambaye anasemekana kuwa na makazi yake maeneo ya Masaki.Amanda alionekana kushtushwa baada ya kuulizwa kuhusu kuwepo kwa picha hizo na kukiri kuwa ni kweli mtu huyo anafahamiana naye. 
Tamrina Poshi maarufu kama Amanda akipozi.

“Duh! hizo picha zimefikaje kwenu? Jamani haya ni maisha yangu binafsi naombeni mniache na huyo jamaa ni rafiki yangu sana, kwanza siyo mtanzania ni raia wa Uturuki,” alisema muigizaji huyo.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top