Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
IMG_0114.JPG
Wakati wapinzani wao wa jadi Real Madrid wakiwa wapi nchini Morocco kushiriki michuano ya kombe la dunia kwa vilabu, FC Barcelona leo imefanikiwa kuisogelea Madrid kileleni na kubakisha pengo la pointi moja tu.
Wakicheza katika dimba lao la Camp Nou, FC Barcelona leo wameiadhibu Cordoba magoli 5-0 katika mchezo wa ligi kuu ya nchi hiyo.
Pedro alianza kufungua ukurasa wa magoli mwanzoni kabisa mwa mchezo, dakika ya 2, goli ambalo lilidumu mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika.
Kipindi cha pili, dakika ya 53, baada ya kusubiri kwa mechi zaidi ya 10, hatimaye mshambuliaji Luis Suarez alifunga goli lake la kwanza katika ligi kuu ya Spain.
Gerard Pique akaongeza goli la 3 dakika ya 80, kabla ya Lionel Messi kufunga mengine mawili dakika ya 82 na 90 na kuhitimisha ushindi wa 5-0.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
20 Dec 2014

Post a Comment

 
Top