March 22, 2025 08:54:41 PM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Hivi inakuwaje pale unapokwenda kwenye ATM kutoa pesa toka kwenye akaunti yako na badala ya pesa kutoka anachomoza nyoka anayejaribu kukuua kwa sumu yake kali?, hiyo imetokea kweli nchini Hispania.

Mwanaume mmoja wa nchini Hispania alinusurika maisha yake baada ya kunusurika kugongwa na nyoka wakati akitoa pesa toka kwenye ATM.

Mwanaume huyo alienda kwenye mashine ya kutoa pesa ATM iliyopo nje ya benki ya Caja Madrid bank katika mji wa Llodio, kaskazini mwa Hispania.

Katika hali ambayo hakuitegemea, zilichomoza pesa sambamba na nyoka ambaye alijaribu kumgonga kwenye mikono yake. Pamoja na hayo jamaa hakuziacha pesa zake zikining'inia kwenye ATM, alizichukua pesa zake kabla kuwapigia simu polisi kuwajulisha juu ya tukio hilo.

Kwa msaada wa meneja wa benki, polisi walifanikiwa kumtoa nyoka huyo na kumweka kwenye boksi ili waweze kumrudisha porini.

Inavyoonekana ni kwamba nyoka huyo huenda aliingia mwenyewe ndani ya ATM kwakuwa ATM hiyo ipo karibu na kichaka.

Angalia VIDEO ya nyoka huyo kwenye ATM wakati polisi akijaribu kumtoa kwa kutumia fimbo. 
kama kifaa chako hakina Uwezo bonyeza Hapa

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
12 Dec 2014

Post a Comment

 
Top