Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Baadhi ya wahusika wa vikosi vya Utafutaji wa ndege hiyo.
Baadhi ya wahusika wa vikosi vya Utafutaji wa ndege hiyo, Indonesia.
Vyombo mbalimbali vya habari vya Kimataifa vimeanza kuripoti kuhusu kinachoendelea kwa sasa katika hatua za utafutaji wa ndege ya AirAsia QZ8501 iliyopotea siku ya juzi December 28 ikitokea Indonesia kwenda Singapore.
Vikosi vya utafutaji vimetoa taarifa kwamba kuna mabaki mbalimbali ya ndege ambayo yamepatikana yakiwa yanaelea juu ya maji ya bahari katika eneo ambalo ndege hiyo ilipoteza mawasiliano.
AirAsia II
Mkurugenzi wa Shirika la anga Indonesia Djoko Murjatmodjo amesema kuna baadhi ya vitu vimeonekana ikiwemo mwili wa mtu mmoja ukiwa unaelea baharini pamoja na mabaki ambayo bado hawajathibitisha kama ni ya ndege hiyo ambayo ni mlango wa abiria na mlango wa sehemu ya kupakilia mizigo.
Mabaki

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top