
Utafiti mpya unasema kwamba wanawake wazee wanaotaka kupata watoto ni sharti watafute vijana wadogo.
Utafiti huo unasema kuwa ijapokuwa wanaume hawana kiwango cha mwisho cha kutafuta watoto,fursa hiyo hupotea kila miaka inavyozidi.
Wakati unapotafuta watoto basi umri wa mwanamume ni muhimu tu kama ule wa mwanamke.
Utafiti huo uliwahoji takriban wanawake 631 walio na umri kati ya 40 na 46 pamoja na wapenzi wao walio na umri kati ya 25 na 70.
Wanawake hao baadaye waligawanywa katika makundi mawili kulingana na iwapo ni wazazi au la.
Utafiti huo pia umebaini kwamba wanawake wengi huanza kukosa kushika mimba wakiwa na miaka 40 huku wanaume nao wakianza kubahatisha wafikapo miaka 43.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment