
Kama unakumbuka vizuri tuliishia pale ambapo mwanamke anamtamani mwanaume mwenye gari ambaye anamtumia kisha anammwaga kisha anatafuta mvulana mwingine ili aendelea kuwa juu kwenye sekta ya starehe kama alivyokuwa awali.
TUENDELEE…
Yule mwanaume mwenye gari anammwaga sababu anaamini kesho atapata mwingine ambaye atakuwa na kiu ya kupenda gari kama alivyolipenda yule wa awali.
Staili ya maisha kwa mwanaume wa dizaini hiyo inakuwa ni ya kupokezana kijiti, maana atakuona hufai, atahamia kwa mwingine.Kwa kuwa na wewe unakuwa umeshazoea maisha ya kujirusha, hutakubali. Utataka kwenda sawa, utatafuta mwingine ambaye naye ana gari au kitu kingine cha anasa ukiamini utakwenda sawa na maisha ya kisasa, kula ujana!
Kwa upande wa wanaume tatizo hili madhara yake ni kutojijenga kwa wakati. Wanatumikia starehe, wanashindwa kujijenga kimaisha.Aina ya maisha anayoishi si rahisi kukutana na mwanamke bora, hakuna atakayekubali kuanzisha naye uhusiano kwa sababu sifa yake inakuwa ni mbaya.
Ujana unakuwa umemtawala kiasi kwamba hafikirii kuhusu ‘future’ yake. Anachowaza ni sehemu gani kuna starehe, atapata wapi mtoto mzuri wa kuburudika naye usiku huo kisha kesho yake atafute mwingine.
Mtu wa aina hiyo, suala la ufujaji wa fedha kamwe halijui, kuweka mikakati ya kutengeneza msingi wa familia yake baadaye ndiyo kabisa, hana muda.Umri utamtupa mkono, ataingia kwenye ndoa akiwa hohehahe. Hata ikitokea hiyo siku anataka kuingia, ataingia kwa sababu tu tayari umri utakuwa umemtupa mkono, hana namna.
Unaporukaruka na ujana katika ulimwengu wa sasa wenye magonjwa mengi, madhara yake ni makubwa likiwemo suala la kupata maambukizi ya magonjwa ya hatari na kujikuta ukijutia
safari yako ya ujana.
Kupenda urahisi
Vijana wengi kwa sasa hawapendi usumbufu hasa katika suala zima la kumsaka mwenzi wa maisha.
Wanapenda kuingia katika penzi lisilo na vikwazo vingi, anataka akutane na mtu leo wamalizane kila mtu ashike hamsini zake.
Athari ya kupenda urahisi inajengeka na kuwa
tabia. Inaanza taratibu lakini baadaye inakomaa kufikia hatua ya kutopenda kabisa ‘usumbufu’ wa kumtafuta mwanamke au mwanaume.
Hapo ndipo kwa
wanaume wanapotumia fedha kununua
wanawake na hata wanawake pia wapo wanaowanunua
wanaume.
Malezi
Kwa kiasi kikubwa familia ambazo vijana wake wanakuwa hawajatulia kwa
kuendekeza starehe kula ujana, huchangiwa na malezi mabaya.
Wakiteleza tu hapo vijana wao huangukia katika tabia ya kubadilibadili wachumba kwa kupenda urahisi.
Tamaa
Matamanio ya kimaumbile ni chanzo cha wengi kutopenda kutulia na mtu. Leo atamuona
huyu amejazia mapaja, kesho atamuona mwenye mwanya mzuri, mara atamuona mwenye macho mazuri naye atakuwa
anahama kulingana na tamaa inavyomuelekeza.
Mtu usipoidhibiti tamaa, matokeo yake ni kuwa mtu wa kurakaruka. Kila msichana mzuri utataka awe wako. Na kwa wanawake vivyo hivyo, kila mwanaume ‘handsome’ au mwenye fedha utataka awe wako.
Ni vyema kujitathimini kupitia sababu hizo na nyinginezo, ishi katika misingi mizuri ili uweze kufikia uzee wako ukiwa na heshima ya ndoa yenye maadili.
Bonyeza Hapa kuungana nasi facebook
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro









Post a Comment
Post a Comment