Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 
Hata Kundi la Wanaume TMK aka ‘wazee wa mapanga shaaa’ lilijichukulia umaarufu mkubwa enzi likiwa na members wote waliolianzisha. hivyo kundi hilo lilikuja kuvunjika na kuzaliwa makundi mawili, Wanaume Halisi linaloongozwa na Juma Nature na TMK Wanaume Family ambalo lipo chini ya Said Fela likiwa na wakali kama Chege na Mheshimiwa Temba. Na sasa imebainika kuwa ni mwanamke ndiye aliyewakosanisha jamaa hao. “Tatizo wote tulivurungwa na ujana mwisho wa siku tukatoa chance kwa watu na wamechukua nafasi,” Fela aliiambia Bongo5.
“Siwezi kusema sio au ndio, lakini huyo mwanamke ameshinda ametushawishi mpaka kubomoa, maana yake ni sawa sawa mwanamke anatumwa kwenda kubomoa nchi. Viongozi kama tunagombania nchi kwa ajili ya mwanamke basi tulifeli sisi upande wetu,” alisisitiza.

Jumatatu hii Mheshimiwa Temba amepost picha ya Wanaume TMK kabla halijameguka na kuandika ‘Kabla shetani hajapita.”
Fela amedai kuwa anapanga kuzungumza na Nature ili waendelee kufanya kazi tena.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top