Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Heroine
Bado taarifa za watu kukamatwa na dawa za kulevya zimeendelea kuchukua nafasi, ni siku chache zimepita tangu Polisi wa Nigeria kumkamata mtu ambaye alikuwa anasafirisha dawa za kulevya akiwa amefisha ndani ya viatu vya kike ndani ya mabegi makubwa mawili, leo kuna watu wengine wane wamekamatwa wakisafirisha mzigo wa dawa hizo.


Polisi wa Mombasa, Kenya wamesema wanawashikilia watu wanne kwa kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroine.
AAskari wa Kenya wakiwa eneo walipowakamata watuhumiwa hao.

Askari Polisi wa Kenya.
Mpelelezi ambaye anafanya kazi na kikosi cha kuzuia Mihadarati, Kenya Anti-narcotics Unit, Hamis Masha amesema watu hao wanadaiwa kuhusika na mifuko 98 za dawa hizo zilizokamatwa Nairobi na walikuwa wakitafutwa na maafisa wa usalama wa Marekani wa DEA.


Maafisa hao wamesema dawa hizo huwa zinasafirishwa kutoka Pakistan na Iran na  kuingia katika bandari za Afrika Mashariki ambako kuna ukaguzi duni wa bidhaa zinazoingizwa na baadaye kupelekwa Ulaya.
Watu hao waliokamatwa wawili wana asili ya Kenya na wawili asili ya India.

Kama Bado Hujajiunga Nasi, Unaweza Kujiunga Hapa Nikutumie habari Moja Kwa Moja ..Bofya  HAPA!..

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top