Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta amesema kilichomkuta aliyekuwa Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya Katiba jana ni sawa na kujitakia mwenyewe.
Akihojiwa muda mfupi uliopita na Redio Voice of Tabora kuhusu maoni yake kwa vurugu kubwa iliyoongozwa na Paul Makonda jana, Mzee Sitta amesema kimsingi wananchi walio wengi wanaunga mkono Katiba pendekezwa.
Mzee Sitta amesema Jaji Warioba anapaswa kutulia kwani akiendelea anaweza kuaibishwa kuliko aliyofanyiwa jana pale Ubungo blue pearl.
Mzee Sitta amemtaka Warioba awaachie wananchi Katiba pendekezwa waamue wenyewe kwa njia ya kura.Sitta ameendelea kusema watanzania wa sasa siyo wajinga na wakikuona unawadanganya watakuvamia hapohapo.Amedai uelewa wa wananchi kwa sasa ni mkubwa kuliko wakati mwingine wowote.
Alipoulizwa swali kuhusu Uvumi kwamba yeye ndiye anamfadhili na kumtuma Paul Makonda kupambana na yeyote anayempinga Mzee Sitta amecheka na kusema hatajibu hilo swali.
Bonyezahapa
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- Profesa Lipumba Asema Hana mpango wa kuhama CUF wala kuanzisha chama Kingine ........Ataja Sababu Zilizomfanya Amkatae Lowassa08 Sep 20160
Aliyekuwa mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amesema hana mpango wa kuhamia chama choch...Read more ?
- Msajili amlima Barua Maalim Seif kuhusu sakata la Lipumba01 Sep 20160
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa nchini imemuandikia barua Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananch...Read more ?
- Breaking News: Mbowe Atangaza Kuahirisha Maandamano ya Oparesheni UKUTA Yaliyokuwa Yamepangwa Kufanyika Kesho31 Aug 20160
Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo ametangaza kusitishwa kwa maandamano ya Opare...Read more ?
- Hotuba ya Edward Lowassa alipokuwa Iringa Jana25 Aug 20160
Leo(Jana) nimewatembelea ndugu zangu wa Kilolo - Iringa kuwashukuru na kuwaeleza kuwa tu...Read more ?
- Prof Lipumba:Sihusiki na Vurugu zilizotokea Katika Mkutano wa CUF23 Aug 20160
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Prof.Ibrahim Lipumba amesema hausiki na fujo wala vurugu zilizotokea ...Read more ?
- Mbunge kizimbani kwa maneno ya uchochezi23 Aug 20160
MBUNGE wa Jimbo la Tanga kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Mussa Mbarouk amefikishwa katika Maha...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment