Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Mtu anayekadiriwa kuwa na umri kati ya 32-40 amenusurika kupoteza maisha katika ajali iliyotokea mjini Moshi asubuhi ya leo ikihusisha polisi, na magari mawili.

Ajali hiyo imetokea barabara ya Boma mjini hapa majira ya saa 3:20 asubuhi ikihusisha gari aina ya Toyota Spacio yenye namba za usajili T 111 BHW na gari jingine aina ya Toyota Corolla yenye namba za usajili T 378 BCL ajali iliyotokea mbele ya jengo la TFA, mkabala na jengo la Vodacom.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema askari wawili walikuwa wakimfukuzia mwenye gari namba T 111 BHW aliyekataa kusimama baada ya kutakiwa na askari hao kusimama mjini hapo, ndipo walipoanza kukimbiza kwa kasi isiyokuwa ya kawaida.

Waliongeza kuwa mwenye gari la Toyota Spacio alipoona mambo yamekuwa magumu akaamua kuliegesha gari katika eneo la maegesho la ofisi za TFA ambapo mwendo wake ulikuwa wa kasi, alipofungia kazi katika gari namba T 378 BCL lililokuwa limeegesha hapo.

Aidha walisema kufuatia kuligonga kwa nyuma gari hilo lililoegeshwa hapo Toyota Spacio ilipaa hewa na kuzunguka mara mbili kama inavyoonekana kwenye picha na kutua chini ambapo dereva ambaye hakufahamika jina lake aliponea chupuchupu.

Ndugu wa dereva walipeana taarifa na kumchukua ndugu yao na kumfikisha katika Hospitali ya KCMC kwa matibabu kutokana na kupata majeraha kidogo sehemu za kichwani.

Hata hivyo waliongeza kuwa maafisa wa jeshi la Polisi mkoani humo waliokuwa wakimkimbiza walibadilisha mada na kuanza kupima ajali hiyo hali waliyooita ni kuvunja sheria kwani polisi hairuhusiwi kulikimbiza gari isipokuwa kwasababu maalum tu.

Maafisa wa jeshi la Polisi walionekana eneo la tukio wakiwa na pikipiki zenye namba PT 2427 na PT 2426 wakiendelea na kazi ya upimaji wa tukio hilo.

Hadi tunaileta habari hii, hali ya mambo katika eneo la tukio “breakdown” namba T 528 ABT aina ya Land Rover ilikuwa katika harakati za kuinua magari hayo ili kuyafikisha kituo cha polisi cha kati mjini Moshi.



Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top