Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu wakiwa katika matembezi ya amani.

Baadhi ya mabango yakiwa na ujumbe tofauti.

Askari polisi wakisimamia ulinzi wa watembeaji hao.

Bi Zainabu Juma, muumini  wa Kiislam akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).
Hivi ndivyo matembezi  yalivyokuwa.
Waumini wa kike wa Kiislam wakiimba.
…Wakiimba na kucheza baada ya matembezi

WAUMINI wa msikiti wa Masjid Ghadiri uliopo Kigogo Post, jijini Dar es Salaam, leo wamefanya matembezi kuanzia Ilala mpaka Kigogo, kwa ajili ya kuhimiza na kuhamasisha amani kwa Watanzania na walimwengu kwa ujumla.

Tarehe 4 Novemba kwa Waislam inajulikana kama siku ya Ashura, siku ambayo ilishuhudia moja ya mihanga adhimu na mikubwa ya wanadamu katika kumbukumbu za kihistoria za kila mwaka. 
Ni siku ambayo, mjukuu wa pili wa Mtukufu Mtume Muhammad (S.A.W.) na watu wa karibu yake waliuawa kikatili  katika jangwa la  Karbala nchini Iraq na miili yao kukatwakatwa  kwa amri ya Yazid bin Muawiyah, mtawala dhalimu wa ulimwengu wa Waislam kwa wakati huo.Hayo yamesemwa na Shehe Hemed Jalala, Imam wa Masjid Ghadiri Kigogo Post alipowaongoza mamia ya waumini katika matembezi hayo.

(Habari/Picha na: Gabriel Ng’osha/GPL)

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top