Ligi kuu ya soka England imeendelea hii leo kwa michezo miwili iliyopigwa kwenye jiji la Manchester na jijini Birmingham ambapo kwenye mchezo wa kwanza Mabingwa watetezi wa ligi hiyo Manchester City waliwafunga mahasimu wao wa jadi Manchester United moja bila kwenye uwanja wa Etihad .
United katika mchezo huo ilimaliza ikiwa pungufu baada ya mlinzi Chris Smallingkuonyeshwa kadi nyekundu mapema kwenye kipindi cha kwanza ambapo hata hivyo matatizo ya United hayakuishia hapo kwani baadaye mlinzi wa kimataifa wa Argentina Marco Rojo alilazimika kutolewa nje baada ya kuumia bega.
Huu ni ushindi wa nne mfululizo ambao City inaupata mbele ya United huku Sergio Aguerro akiendelea kuwaumiza mashetani wekundu akiwa tayari amefunga magoli matano kwenye michezo sita dhidi ya United.
Matokeo Mengine
Matokeo Mengine

Bonyeza hapa
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment