Stori: Waandishi Wetu
Imefichuka! Kwa muda mrefu kumekuwa na taarifa za chini kwa chini kwamba baadhi ya mastaa wa kike Bongo, hasa wale wa filamu ‘Bongo Movies’ huuzwa kwa wanaume, mara nyingine kwa kujua au kutojua lakini wenyewe wamekuwa wakikanusha hivyo kutoa ‘kibarua’ kwa Ijumaa kuingia mzigoni kisha kumuibua mmoja wa wahusika (kuwadi) anayerahisisha biashara hiyo haramu ya ngono.
Jokate Mwegelo akipozi.
UCHUNGUZI
Uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kwamba, kuwadi huyo huwa anajua dau la kila staa hivyo anapopata mwanaume hasa mapedeshee, wafanyabiashara na baadhi ya vigogo serikalini, huwaunganisha kwa kutoa namna ya mawasiliano au kuwaunganisha moja kwa moja.
MADAI MAZITO
Uchunguzi huo ulibaini uwepo wa madai mazito kwamba wapo baadhi ya mastaa wa kike wa Bongo Movies ambao hugombewa na makuwadi kwa sababu wana soko kubwa.
“Jaribu kufikiri msanii haonekani location (eneo la kuigizia sinema) wala sinema aliyocheza haijulikani lakini muda mwingi utamuona anatanua kwenye viwanja vya starehe, lazima ujiongeze kwamba kipato kinatoka wapi?
Staa wa filamu Bongo Aunt Lulu.
“Mimi nakwambia hii Bongo Movies imebaki jina tu, sioni mwanga mbeleni kwa sababu hawa mabinti hawapo serious zaidi ya kutafutiwa wanaume,” kilidai chanzo chetu ambacho ni mfuatiliaji wa karibu wa kazi za sanaa Bongo.
STAA GANI MWENYE SOKO KUBWA?
Madai mazito yaliendelea kushushwa kwamba wapo wanunuaji ambao huhonga magari (bila kadi) ambapo baadaye hukamatwa kimafia na kurejeshwa kwa mhongaji.
Ikazidi kufahamika kwamba, mastaa wenye sifa ya kuhongwa magari ni wale wenye majina makubwa.
Staa wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper Massawe.
KUANZIA SH. MIL. 5 HADI BUKU 50
Ilisemekana kwamba wapo mastaa wanaotajiwa dau kubwa kuanzia Sh. milioni tano na kuendelea na wapo wa chini ya hapo hadi buku hamsini (50,000).
Mpaka sasa kuna mastaa wanaowindwa na makuwadi kwa kuwa wana soko na bei zao kwenye mabano ni pamoja na Elizabeth Michael ‘Lulu’ (Mil. 5), Jokate Mwegelo (Mil. 5), Wema Isaac Sepetu (Mil. 5), Kajala Masanja (Mil. 5) na Jacqueline Wolper Massawe (Mil. 5).
Staa wa filamu Bongo, Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’.
Wengine ni Baby Joseph Madaha (Mil. 5), Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ (Mil. 3), Aunty Ezekiel (Mil. 3), Jennifer Mwaipaja ‘Shumileta’ (Mil. 2) Isabela Francis ‘Vai wa Ukweli’ (Mil. 1), Lulu Mathias ‘Anti Lulu’ (Mil. 1), Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’ (Mi. 1) na wengine kibao ambapo kwa sasa upepo umegeukia kwa wale wanaochipukia.
ANAYEWAUZA MASTAA HUYU!
Katika kusaka ukweli juu ya skendo hiyo, jina la mmoja wa makuwadi hao ambaye ni mwigizaji wa kike Bongo, Lungi Maulanga (pichani) ilitajwa.
Staa wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Mbali na Lungi pia alitajwa mwigizaji mmoja wa kiume wa Bongo Movies na jamaa mwingine ambaye huwa ni mdandiaji wa ishu za mastaa (majina tunayo, tutayataja tukijiridhisha kisheria).
LUNGI ASAKWA
Baada ya kutajiwa jina la Lungi, gazeti hili lilimsaka mwigizaji huyo anayedaiwa kuwauza baadhi ya mastaa hao kwa wanaume ambapo alibanwa vilivyo hadi akaanika siri nzito nyuma ya biashara hiyo kubwa isiyo na kodi.
Staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu.
Mbali na kukiri kuwakuwadia mastaa hao kipindi cha nyuma kabla ya kuacha, Lungi alifunguka kwamba amekuwa akisumbuliwa na wanaume wakware wakitaka awaunganishe na mastaa ambao alidai alishafanya nao kazi hiyo muda mrefu.
MSIKIE LUNGI
Ijumaa: Habari yako Lungi...
Lungi: Nzuri, mmekuja kufuata nini hapa (nyumbani kwake Kinondoni, Dar)?
Ijumaa: Mbona unajihami? Tumekuja kukusomea mashitaka yako!
Lungi: Mashitaka gani? Siku hizi nimetulia, sijichanganyi kama zamani, kulikoni tena?
Ijumaa: Hapa kuna madai mazito...
Staa wa filamu Bongo, Vai wa Ukweli.
Lungi: Hebu semeni kilichowaleta, kwanza siku hizi sipendi kukutana na waandishi wa habari!
Ijumaa: Kuna za chinichini kwamba wewe ndiye unayewauza mastaa wa Bongo na ndiyo biashara inayokuweka mjini kwa kuwa hata location huonekani. Je, ni kweli?
Lungi: (kwa hasira) yaani mimi niwekwe mjini na mastaa? Kwani hamjui anayeniweka mjini? Au mnataka niwafukuze na panga?Ijumaa: Kwa nini unakuwa mkali Lungi? Unachotakiwa kufanya ni kutoa majibu kwa sababu kuna shosti’ako ametutajia staa uliyemuuza juzi tu!
Staa wa filamu Bongo, Aunty Ezekiel akipozi.
Lungi: (bila kujua anarekodiwa) juzi! Sikieni, nawaheshimu sana, mimi nilikuwa nikifanya biashara hiyo siku nyingi na niliacha kwa sababu hao mastaa hawana maana, wakishapata wanajisikia na kusahau walipotoka.
“Huyo aliyewaambia ana ushahidi gani kama juzi nimeshamuuza staa?
Ijumaa: Oke, tuache hilo! Unakumbuka dau kubwa ulilowahi kupewa wakati unawakuwadia?
Lungi: (kwa mara ya kwanza anatabasamu) nilishawahi kupata hadi Sh. milioni tatu na kima cha chini laki tano, lakini jamani mbona ni siku nyingi?
Staa wa filamu Bongo, Lungi Maulanga.
“Kwanza mimi sitaki hizo habari kabisa. Nimechoka kusumbuliwa na wanaume kwa ishu hizo.”
Ijumaa: Hilo dau kubwa ulilipata kwa mwanaume wa Dar, mikoani au nje ya nchi?
Lungi: Watu wa mikoani ndiyo wanakata mkwanja mkubwa, hapa Dar longolongo tu. Hiyo Sh. milioni tatu niliipata kwa jamaa mmoja wa Arusha.
Chanzo Global
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- Mfungo Wamuepusha Amanda na Skendo...'Mwezi Huu Nguo Fupi za Kuwatega Wanaume Nimeziweka Pembeni'01 Jul 20150
Staa wa bongo movies, Tamrina Posh ‘Amanda’ amesema kuwa mfungo wa mwezi wa ramadhan...Read more ?
- Jingine Laibuka Kuhusu Rais wa FIFA..Kumbe Pia Alikuwa Anakula Demu wa Mchezaji Cristiano Ronaldo06 Jun 20150
Hali bado sio shwari kwa upande wa Rais wa FIFA, Sepp Blatter… Zimepita siku chache tu tangu atan...Read more ?
- Wellu Sengo Adaiwa Kutoka na Mume wa Mtu Mwigizaji Mwenzake Steven Nyerere02 May 20150
Mrekebishatabia wa Insta ameibua Mazito Kama ifuatavyoSaaaasa????? @stevenyerere2 ndo umeoa mke ...Read more ?
- Aunt Ezekiel Atoboa Kuhusu Wasanii wa Bongo Movies Kujitengenezea ‘Skendo’22 Apr 20150
Staa mrembo wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel ‘Mama Kijacho’ amesema baadhi ya wasanii wa bongo movie...Read more ?
- Kipa wa Simba JR MANYIKA 'Anae Sema Naima Ananiua Kiwango Aje Acheze yeye Mimi Sio Khanisi Nina Haki ya Kuwa na Mpenzi'21 Apr 20150
BAADA ya Simba kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Mbeya City katika mechi ya ligi kuu soka Tanzania bar...Read more ?
- Mume wa Mtu Apiga Picha za Utupu na Mchepuko..Picha Zasambaa Mtandaoni07 Mar 20150
KALOLI Dawa ambaye ni mume wa mtu, amedaiwa kujipiga picha za utupu akiwa na mchepuko wake uliofa...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment