Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Stori:  Erick Evarist na Musa Mateja
MIEZI michache kufuatia tamko la serikali  kuzuia ngoma zinazokesha maarafu kama Kanga Moko kwa kukiuka maadili, imebainika kuwa ngoma hizo zinaendelea kufanya mambo kama kawa kana kwamba hazijakatazwa, Ijumaa limeshuhudia.

Baadhi ya wadada wakicheza ngoma ya kibao kata wakiwa ndani ya kanga moja.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili juzikati umebaini kuwa ngoma hizo ambazo wanawake hucheza wakiwa ndani ya kanga moja, zinaendelea kufanyika kwa siri katika viunga mbalimbali vya Jiji la Dar es Salaam.Chanzo makini kimevujisha habari kuwa, wahusika wamekuwa wakipashana habari kupitia kwenye mitandao ya kijamii kisha kukutana katika maeneo tulivu hasa kwenye fukwe na kufanya yao.
Wadada hao wakicheza ngoma hiyo huku wakipata sapoti kutoka kwa shabiki wa mchezo huo.
“Siku hizi wanatangaziana kwenye mitandao ya kijamii kisha mashabiki na wadau wakubwa wa ngoma hizo wanakwenda kuwashuhudia,” kilisema chanzo.Kuonesha kwamba kipo ‘serious’, chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kwa kunyetisha siku ambayo ngoma hizo zilifanyika katika ufukwe mmoja uliopo Mikocheni jijini Dar.

Wengine walishiriki mashindano ya umiss.
“Jumamosi hii (iliyopita) watafanya mambo yao katika ufukwe wa...(anautaja jina) uliopo maeneo ya Mikocheni, kama mtaweza fikeni muone jinsi usiku unavyotumika vibaya na ngoma hiyo,” kilisema chanzo hicho.
Wadada hao wakizidi kutoa shoo.
Siku ya tukio, mapaparazi wetu walitinga katika ufukwe huo na kujionea wadada watatu wakionesha ufundi wa kucheza ngoma hiyo wakiwa wamevalia kanga moja kama kawaida yao.Mara baada ya mapaparazi wetu kunasa picha kadhaa, walijaribu kuwauliza wadada hao kwa nini wanakaidi agizo la serikali, lakini hawakuwa tayari kuzungumza lolote.
Ma DJ wakinogesha 'beach party' hiyo.
Mapema mwaka huu, Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), lilipiga marufuku ngoma hizo kwa kuonekana hazina maadili na si utamaduni wa Mtanzania.
Chanzo Global

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top