Basi la kwanza nchini Uingereza linalotumia kinyesi na uchafu unaotokana na chakula limeanza safari yake ya kwanza.
Bio
Bus,lenye viti 40 na ambalo linatoa huduma ya uchukuzi kati ya Bath na
uwanja wa ndege wa Bristol ,linaweza kusafiri hadi maili 186 kwa kutumia
tangi moja la gesi.
Gesi hiyo hupatikana kupitia kutibu maji taka na uchafu wa chakula usiofaa kwa matumizi ya binaadamu.
Uchafu
unaopatikana katika abiria wa basi moja unaweza kutumiwa kutoa kawi ya
kulisafarisha basi hilo kutoka Lands End hadi John O'Groats.
Basi
hilo ambalo limepewa majina kadhaa ya kutungwa likiwemo lile la Basi la
pili linapongezwa kama njia mojawapo ya kuchochea usafiri wa uma huku
ukiimarisha ubora wa hewa jijini.
Gasi inayotumiwa kuliendesha
gari hilo hutoka katika mradi wa maji taka wa Bristol ambao husimamiwa
na GENeco ambyo ni kampuni tanzu ya Wassex Water.
Mohammed
saddiq,meneja mkurugenzi wa kampuni ya GENeco ,anaamini chakula na maji
taka yanaweza kutoa kawi ya Biomethane inayotoa gesi katika shirika la
kitaiafa la gesi inayoweza kutoa gesi yenye uwezo wa kutumika katika
nyumba 8,500 mbali na kuliendesha basi hilo la Bio.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment