Kikao cha Bunge kinaendelea Dodoma leo Novemba 25, kuna Wabunge ambao waliomba miongozo kwamba suala la mjadala wa Escrow limefikishwa Mahakamani, ambapo walilalamika kwamba kitendo hicho kitazuia Bunge kujadili kuhusu Ripoti ya CAG ambayo iko mikononi mwa kamati ya PAC.
Kutipia mtandao wa Twitter kituo cha ITV (@ITVTANZANIA) kiliripoti taarifa ilisoeomeka hivi;-
“#Habari Maafisa wanao jitambulisha kuwakilisha PAP wapo mahakama kuu ya DSM kufungua shauri la kuzuia suala la Escrow kujadiliwa na Bunge.”
“#Habari PAP wamefungua shauri namba 50 ya 2014 mahakama kuu kanda ya DSM wanamshitaki waziri Mkuu,Spika,CAG,na katibu wa bunge.”
Mbunge John Cheyo aliuliza kuhusu suala hilo; “…Tumepata taarifa kwamba jambo ambalo Bunge lako linashughulikia sasa, linapelekwa Mahakamani na dhana ya kuzuia Bunge hili lisifanye kazi yake. Sasa watu wengine kwa ujanja ujanja wanalipeleka Mahakamani ili Bunge hili lisifanye kazi yake, hata kama hujapokea hizo taarifa niko tayari kukupelekea kwa baadaye ili uweze ukatoa mwongozo unaostahili…”
Spika Makinda akajibu; “…Nyie waheshimiwa Wabunge msianze kuishi kwa wasiwasi, sisi kinga zetu ziko wazi hakuna mtu anayeweza kutushtaki sisi tusifanye kazi yetu, hayupo. Hayupo mtu atakayezuia sisi tusifanye kazi za Kibunge na kazi ambazo zinatokana na kazi zinazopatikana katika maeneo mnayopita. Kwa hiyo, hiyo shughuli haipo hatuwezi kushtakiwa na nitagawa ile Ripoti niliyosema nitawagawieni humu ndani kwa majina, Ripoti ya Mkaguzi itagawiwa humu ndani kwa majina…”
Kusikiliza mjadala huo, nimekurekodia, unaweza kusikiliza hapa mtu wangu. Credit millardayoFacebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment