Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Hiace iliyopata ajali ikiwa eneo la tukio huku ikiwa imeharibika vibaya

Wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la tukio

Gari ikiondolewa eneo la tukio

Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Dkt Anselm Tarimo akiwa na maafisa wa polisi mkoa wa Shinyanga eneo la tukio
Wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la tukio
Watu watano wanadaiwa kupoteza maisha  leo majira ya saa tano asubuhi baada ya gari ndogo Hiace yenye namba za usajili T761 CKD ikitoka Kahama kwenda Shinyanga Mjini kupinduka katika eneo la Kona ya Buhangija mjini Shinyanga.

Walioshuhudia wanasema hiace hiyo ilikuwa katika mwendo kasi ikifukuzana na Hiace nyingine ndipo ikamshinda dereva wake baada ya kupiga Bamz ya Buhangija na kupinduka mara tatu.

Mashuhuda wa ajali hiyo wanasema wameondoa miili mitano ya marehemu katika gari hiyo.
Majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.

Tutakuletea taarifa kamili hivi punde kuhusu idadi kamiliya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo na idadi ya majeruhi.

Chanzo Malunde1 blog

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top