Kijana mmoja Nicholas Mhagama (25), mkazi wa Makongo Juu Dar, juzi kati alijilipua na mafuta ya taa kisa kikidaiwa kunyanyaswa na babu yake. Tukio hilo lilitokea eneo la Makongo Juu Makaburini usiku ambapo kijana huyo na babu yake aliyemtaja kwa jina moja la Mhagama waligombana.
Kijana Nicholas Mhagama (25) aliyejilipuwa na mafuta ya taa akidai kunyanyaswa.
AJILIPUA KWA MAFUTA YA TAA
Baada ya kijana huyo kuona isiwe tabu alijilipua na mafuta ya taa alipoona maumivu yanazidi akaanza kupiga kelele za kuomba msaada ambapo aliokolewa na kupelekwa Hospitali ya Mwananyamala na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya hali yake kuwa mbaya.
Waandishi walikwenda kufanya mahojiano naye hospitalini hapo ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Ndugu zangu naomba mnisaidie nipone kwani uamuzi niliouchukua haukuwa sahihi ni hasira za kilevi nilichokuwa nimekunywa.
“Yote haya ni sababu ya manyanyaso niliyopata kutoka kwa babu yangu ambaye alinifukuza nyumbani na kunitaka nikapange nyumba wakati nilikuwa na matatizo ambayo alikuwa akiyajua,” alisema Mhagama.
ALIAMBIWA AKICHELEWA ATAFUNGIWA MLANGO
“Siku ya tukio nilimuaga naenda kwa baba yangu mdogo kumsalimia akaniambia nikirudi usiku nitakuta amefunga mlango nitafute pa kwenda kulala.
“Kweli, niliporudi alianza kuninyanyasa kwa maneno, ugomvi wetu ukawa mkubwa nikaona bora nijiondoe duniani kwani siwezi kuendelea kuishi maisha ya manyanyaso kama haya,” alisema Nicholas kwa shida kutokana na majeraha aliyonayo mwilini hasa usoni na mikononi.
Nicholas Mhagama akiuguza majeraha hospitalini.
Akizungumza kwa njia ya simu bibi wa kijana huyo, Bi. Mhagama alikiri kwamba ni kweli huyo babu ambaye yeye anamuita shemeji amekuwa akimnyanyasa sana Nicholas. “Ni kweli amekuwa akimfukuza nyumbani hapo wakati siyo kwake na siku ya tukio baada ya kuona ugomvi umekuwa mkubwa nilikimbilia kwa mwanangu huko Kimara.
“Ugomvi kati ya babu yake huyo mdogo na huyu Nicholas ulianza saa tatu usiku. Nilipoona kero niliamua kutimkia Kimara kwa mwanangu,” alisema bibi huyo.
SIMU YA MOTO YAPIGWA USIKU
“Ilipotimia saa nne usiku nikapigiwa simu na kufahamishwa kuwa Nicholas kajilipua kwa mafuta ya taa.
BABU ORIJINO ALISHAFARIKI
“Mume wangu (Babu orijino) alishafariki na huyu Nicholas kweli kabisa huwa anagombana na huyo babu ambaye ni shemeji yangu. “Kisa cha ugomvi wao ni kumpa manyanyaso ya hali ya juu, nawaomba mumsaidie huyo kijana, naombeni jamani,” alisema bibi huyo.
Bonyeza Hapa
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- Tetemeko Lililotokea Jana Katika Mikoa Ya Kanda ya Ziwa Limeua Zaidi ya Watu 10 na Kujeruhi Wengine 12011 Sep 20160
Tetemeko la ukubwa wa mtikisiko wa kipimo cha Ritcher 5.7 limetokea katika mikoa mitatu nc...Read more ?
- Msafara wa Makamu wa Rais, Samia Suluhu wapata ajali Mtwara.09 Sep 20160
Msafara wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Mama Samia Suluhu Hassan ambao uliku...Read more ?
- Polisi Washuhudia Majambazi Yakitwangana Risasi.......Zakamatwa Shehena za Silaha na Vifaa vya Uhalifu06 Sep 20160
WATU watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wa kutumia silaha, ambao wamehusika kufanya matukio ...Read more ?
- Askari Magereza Atiwa Mbaroni Kwa Kuingia Wodini Akiwa Amelewa na Kisha Kuanza Kufyatua Risasi28 Aug 20160
POLISI mkoani Rukwa inamshikilia askari Magereza, Cleophas Chapaulinge kwa kosa la kulewa na k...Read more ?
- Polisi Mwingine Auawa Kwenye Mapambano Makali na Majambazi Huko Mkuranga27 Aug 20160
Ilikuwa ni kama filamu ya askari na maadui wakati askari wa Jeshi la Polisi walipopambana na wat...Read more ?
- RC Makonda: Polisi Mkikuta Mtu Yeyote Msituni Pigeni bila Huruma.......Haki za binadamu Wakiwauliza Waambieni waje Kwangu26 Aug 20160
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameliagiza Jeshi la Polisi kuwagonga na kuwapiga wah...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment