Richard
Mileski (60), aliyekuwa mmiliki wa hifadhi ya wanyama pori nchini
Mexico ameuawa kikatili na ngamia aliyekuwa akimfuga katika hifadhi hiyo
kutokana na kutompatia ngamia huyo ‘dozi’ ya soda aliyomzoesha
kumpatia.
Taarifa kutoka mtandao wa
rt.com
zinasema ngamia huyo alimvamia Mileski ndani ya hifadhi hiyo na kumpiga
mpaka kuishiwa nguvu, na baada ya kuanguka chini ngamia huyo alimkalia
juu yake kitendo kilichopelekea mtu huyo kufariki.
Maafisa usalama waliofika katika eneo hilo, walilazimika kumfunga
kamba ngamia huyo na kumvuta kwa gari ndogo ili waweze kuutoa mwili wa
marehemu huyo.
Taarifa za awali zinasema huenda ngamia huyo alikasirishwa na kitendo
cha Mileski kutompatia soda aina ya Coca cola alichozoea kumpatia.
Mileski alianzisha hifadhi hiyo maalum aliyoipa jina la ‘Tulum Monkey Sanctuary’
kwa ajili ya kuhifadhi nyani na buibui ambao walikuwa wakitoweka nchini
humo, na baadaye aliongeza wanyama wengine, japo serikali imesema
alianzisha hifadhi hiyo bila ya kuwa kibali wala leseni.
Richard Mileski, mmiliki wa hifadhi aliyeuawa na ngamia.
Kwa miaka 15 Mileski amejitolea maisha yake kwa kuhifadhi wanyama
katika hifadhi hiyo iliyojizolea umaarufu kwa shughuli za utalii.
Mtandao wa China.org.cn wa China umemtaja ngamia huyu ni mnyama wa kwanza kufanya mauaji ya kikatili zaidi duniani.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- Kijana Mwingine Mweusi Auawa Nchini Marekani24 Dec 20140
Eneo la tukio maandamano makubwa yametokea nchini Marekani katika mji wa St Louis yaliyosababis...Read more ?
- Wanajeshi 54 wa Nigeria Wahukumiwa Kifo kwa Kushindwa kupambana na Boko Haram.18 Dec 20140
Mahakama moja ya kijeshi nchini Nigeria imewahukumu kifo askari 54 kwa kukataa kupigana na kundi...Read more ?
- Watu 3 wauawa katika vita nchini Somalia13 Dec 20140
Mwanajeshi wa serikali ya Somali .Vita vimezuka katika ya wanajeshi wa somali na wanamgambo wa Alh...Read more ?
- Milipuko Wiliwi Yaua Watu 30 Nchini Nigeria12 Dec 20140
(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({}); Waokoaji na wakazi wakikutana katika e...Read more ?
- Al Jazeera yaihusisha Kenya na mauaji ya Viongozi wa Kiislamu09 Dec 20140
(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({}); Abubakar Shariff Makaburi ni mmoja wa vio...Read more ?
- Mtoto wa Malkia wa Uingereza kwa mara ya kwanza ndani ya ‘White House’ ya Marekani09 Dec 20140
(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({}); Familia ya Kifalme ya Prince Willium na...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment