MWANAFUNZI
wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Ugalla, Wilaya ya Mlele Mkoa
wa Katavi, Yohana Ramadhani (14), ameliwa na Mamba wakati akioga na
wenzake katika mto Ugalla.
Kwa
mujibu wa Diwani wa Kata ya Ugalla, Mohamed Asenga, tukio hilo
lilitokea Oktoba 18 mwaka huu, saa 11:00 jioni katika mto huo.
Alisema siku hiyo, marehemu akiwa na watoto wenzake kamailivyo kawaida yake, alikwenda kwenye mto huu kwa lengo la kuogelea.
Asenga
alisema kuwa, wakati watoto hao wakiendelea kuogelea, alitokea mama
mmoja aliyefika mtoni hapo kwa ajili ya kuteka maji, ambapo akiwa
anaendelea, alimwona mamba kando ya mto akiwavizia watoto hao pasipo wao
kujua.
Kwamba, mama yule aliwaambia waache kuogelea na watoke haraka ndani ya mto kwani amemwona mamba akiwa pembeni akiwavizia.
“Watoto
hao walitoka ndani ya mto lakini wakati wakiondoka mamba huyo
aliyekuwa pembezoni mwa mto, alimkamata Yohane na kuingia naye mtoni
tena,” alisema na kuongeza kwamba zilipiga yowe kuomba msaada ambapo
wananchi walijitokeza japo hawakufanikiwa kumuokoa.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment