Mahabusi
Daniel Alfred katika kituo cha Polisi Urafiki, eneo la Ubungo,
amefariki dunia kwa madai ya kupigwa na baadhi ya askari wa kituo hicho.Alfred aliyekuwa mkazi wa Sinza jijini hapa, alifikishwa kituoni hapo kwa kosa la wizi wa kuaminiwa na kuwekwa mahabusu wakati akisubiri kufikishwa mahakamani juzi(Jumatatu) ili kusomewa mashitaka yake.
Kamanda Wambura alisema kuwa baada ya kifo chake waliupeleka mwili wake hospitali.
Wambura alisema ripoti ya daktari baada ya uchunguzi, ilionyesha kwamba mahabusi huyo alikuwa mgonjwa.
Shuhuda ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini, alisema alikwenda kituo hapo kumuona ndugu yake lakini alikuta askari wakimpiga.
Alisema hata kama kijana huyo alikuwa mgonjwa, anaimani kuwa aliuawa na polisi kwa kipigo kikali.
Source:Mwananchi
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment