March 19, 2025 06:54:03 PM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Kajala Masanja amekanusha uvumi ulioandikwa kwenye magazeti ya udaku kuwa amefungua kesi dhidi ya mama yake mzazi na Wema Sepetu kutokana kile kilichodaiwa kutukanwa na mama huyo kwenye sherehe ya siku ya kuzaliwa ya Wema mwishoni mwa mwezi uliopita. 


Kajala ambaye amesema yupo busy na kazi zake binafsi, ameiambia Bongo5 hana ugomvi wowote na Wema kama watu wanavyozusha. β€œHapana sijamfungulia mashtaka yoyote Mama Wema. Siwezi kufanya kitu kama hicho mama ni mzazi, mzazi kama mzazi huwezi ukasema umrudishie kitu,” amesema. β€œMzazi anaweza akakutukana akakufanyia nini lakini still atabakia kuwa mzazi. Sina ugomvi wowote na Wema, hayo mambo sasa hivi hayapo ni kazi tu.”



                              Wema na mama yake

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
10 Oct 2014

Post a Comment

 
Top