Home
»
Matukio
» Baba Levo apata ajali akiwa ndani ya basi la AM lililogongana Uso kwa Uso na Coaster
Ni saa tisa kasoro mchana Msanii wa bongofleva Baba Levo anaongea na Millardayo kuongea kwa tabu kwenye usikivu ulio mdogo na kusema kwamba amepata ajali kwenye pori karibu na eneo linaitwa Uluwila akiwa anatokea Tabora kwenda Mpanda.
Alikua kwenye Basi liitwalo AM ambapo ghafla wakiwa kwenye kona ilitokea Coaster ikiwa na abiria ambayo dereva wake alikua akikwepa barabara mbovu hivyo ikabidi ahamie kwenye upande wa pili wa barabara ambako ndiko lilikua linapita basi la kina Baba Levo ambalo hakuliona sababu ni kwenye kona.
Dereva wa basi la kina Baba Levo ilibidi ahame upande wake ili ahamie kwenye upande wa magari yanayopanda ambao ndio upande sahihi wa ile Coaster kupita ambapo juhudi zake hazikufanikiwa kwani wote walikua kwenye spidi na yule dereva wa Coaster alihama kwenye ule upande baada ya kuona atagongana uso kwa uso na basi la kina Baba Levo ila bahati mbaya wakawa wote wamejikuta upande mmoja na wakagongana uso kwa uso.
Mwenye makosa anatajwa kuwa ni mwenye Coaster ambapo pamoja na Baba Levo kuumia usoni na mwilini kwa kuchanwachanwa na vioo vya mbele vilivyopasuka kwenye basi, ameweza kuona kuna baadhi ya watu wamefariki ambapo kati yao ni waliopasuka vichwa na shingo.
Dereva wa basi la kina Baba Levo hajaumia sana wala basi halijaumia sana, Coaster ndio imefumuka upande wa juu wote na kuharibika sehemu nyingine pia huku kilichosababisha Baba Levo kuumia ni kwamba alikua amekaa pale juu ya Injini ya Basi kwenye kigodoro kutokana na basi hilo kujaa.
Baba levo anajisikia vibaya kiasi na kwa sasa yuko na wenzake kama 20 pamoja na Askari mwenye silaha waliekua pamoja kwenye Basi…. wanatembea kutafuta kijiji chenye network ili kuomba msaada manake baadhi ya abiria wamebanwa kwenye hiyo Coaster na hawajatolewa.
Source Millardayo
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- Tetemeko Lililotokea Jana Katika Mikoa Ya Kanda ya Ziwa Limeua Zaidi ya Watu 10 na Kujeruhi Wengine 12011 Sep 20160
Tetemeko la ukubwa wa mtikisiko wa kipimo cha Ritcher 5.7 limetokea katika mikoa mitatu nc...Read more ?
- Msafara wa Makamu wa Rais, Samia Suluhu wapata ajali Mtwara.09 Sep 20160
Msafara wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Mama Samia Suluhu Hassan ambao uliku...Read more ?
- Polisi Washuhudia Majambazi Yakitwangana Risasi.......Zakamatwa Shehena za Silaha na Vifaa vya Uhalifu06 Sep 20160
WATU watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wa kutumia silaha, ambao wamehusika kufanya matukio ...Read more ?
- Askari Magereza Atiwa Mbaroni Kwa Kuingia Wodini Akiwa Amelewa na Kisha Kuanza Kufyatua Risasi28 Aug 20160
POLISI mkoani Rukwa inamshikilia askari Magereza, Cleophas Chapaulinge kwa kosa la kulewa na k...Read more ?
- Polisi Mwingine Auawa Kwenye Mapambano Makali na Majambazi Huko Mkuranga27 Aug 20160
Ilikuwa ni kama filamu ya askari na maadui wakati askari wa Jeshi la Polisi walipopambana na wat...Read more ?
- RC Makonda: Polisi Mkikuta Mtu Yeyote Msituni Pigeni bila Huruma.......Haki za binadamu Wakiwauliza Waambieni waje Kwangu26 Aug 20160
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameliagiza Jeshi la Polisi kuwagonga na kuwapiga wah...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment