Daktari wa jijini New York, aliyetibu wagonjwa wa Ebola Afrika Magharibi amepatikana na virusi vya Ebola hali iliyosababisha hofu ya kuendelea kusambaa kwa ugonjwa huo.

Spencer, 33, alikuwa akifanya kazi na shirika la misaada ya kibinadamu la Medicins Sans Frontieres (MSF) nchini Guinea ambako mamia wamefariki kwa Ebola.
Alianza kuonesha dalili ya Ebola Alhamis asubuhi na alitolewa nyumbani kwake huko Manhattan na kuwekwa kwenye eneo lililotengwa la hospitali ya Bellevue na timu iliyokuwa imevaa nguo rasmi.
Uthibitisho wa vipimo vyake vya Ebola umesababisha hofu kubwa ya kusambaa zaidi kwa ugonjwa huo ambao hadi sasa umesababisha vifo vya karibu watu 4,900 wengi kutoka Liberia, Sierra Leone na Guinea.
Kibonajoro.com ndio mtandao wako kwa habari za ndani na nje, Tuwe pamoja huku pia >> Facebook
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment