Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Nuh Mziwanda jana alijikuta katika wakati mgumu mjini Tabora baada ya Shilole kuwauliza wakazi wa mkoa huo anakotokea iwapo Nuh Mziwanda anafaa kuwa mume wake.
Shilole wakiwa amebambiwa na mpenzi wake Nuh


Shilole akiwa amebambiwa na mpenzi wake Nuh

Shilole ambaye ni mchumba wa Nuh alifunguka mbele ya mashabiki wa Tabora waliokuwa wamefurika kushuhudia show ya Serengeti Fiesta kutaka kujua kama wanamtaka Nuh Mziwanda awe shemeji yao kitu ambacho mashabiki hao walikataa. Mbaya zaidi kwa Nuh, mashabiki hao walimpendekeza DJ Zero kuwa ndiye mwanaume wanayemtaka awe shemeji yake. Shilole aliwajibu wakazi hao kuwa hata wafanyaje yeye binafsi anampenda dogo dogo wake Nuh.
Nuh ambaye kauli hiyo ya shemeji zake wa Tabora ilimnyong’ozesha magoti, ameiambia Bongo5 kuwa wale ni mashabiki tu hivyo Shilole ataendelea kuwa mpenzi wake na anatarajia ‘kuput the ring on it (kwa sauti ya Queen Bey) aka kumvalisha pete ya uchumba Shilole.
Nuh mziwanda
“Unajua mashabiki ni watu na zile kauli walizotoa haziwezi kurudisha nyuma kauli yangu kutompenda Shilole,” amesema Nuh. “Bado ni baby wangu, na kuna mambo mengi yatakuja. Ndioa maana baada ya kuona wanapiga kelele nikaamua kuwatuliza kwa pesa na mwishowe mambo yakaenda sawa. Unajua ingawa watu wanasema mengi juu yetu kiukweli sisi tunapendana na hivi karibuni nitamvalisha pete ya uchumba.”
Credit Bongo5
Like page yetu bonyeza Hapa

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top