Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Dar es Salaam, Tanzania. Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe ambaye ni Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA  hivi punde ametangaza maandamano nchi nzima kushinikiza Bunge Maalumu la Katiba kusitisha shughuli za Bunge hilo kwa kuwa kuendelea kwa Bunge hilo ni kula fedha za wananchi.

“Haiwezekani Bunge Maalumu la Katiba linaendea huku Sitta akiamua kila kitu na kubadlisha kanuni kama yeye ndiyo Rais, Haiwezekani. Nawataka viongozi wenzangu kuandaa maandamo, tena yaelekezwe katika ukumbi wa Bunge kwa mabango,” amesema Mbowe hivi punde.
Mbowe ametoa uamuzi huo mgumu kwenye Mkutano Mkuu wa Chadema unaoendelea sasa kwenye Ukumbi wa Mikutano Mlimani City jijini Dar es Salaam ambako mabalozi wa nchi mbalimbali duniani na viongozi wa vyama vya siasa nchini wamealikwa. Viongozi wa vyama vya siasa walioalikwa ni; Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba, Mwenyekitiwa wa NLD, Emmanuel Makaidi, Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Philip Mangula, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia na viongozi wengine.
Akizungumzia suala la UKAWA amesema vikao vya Bunge vinavyoendelea bungeni ni wizi wa fedha za wananchi na aliwahoji wajumbe kama wako tayari kwa uamuzi mgumu na bila kuchelewa walisimama na kuitikia kwamba  wako tayari.
 Katika hotuba yake Mbowe ametaka kusimamishwa kwa vikao vya Bunge Maalumu la Katiba kwa kuwa kuendelea ni kupoteza fedha za wananchi.
Amesema kama hayo yasipotekelezwa basi UKAWA itafanya maandamazo nchi nzima na amewaangiza viongozi wenzake wa UKAWA kila mkoa kuandaa maandamano hayo kwa kutumia pikipiki, daladala na vyombo vingine.
 “Najua kuwa maandamano yana gharama zake, lakini demokrasia ya kweli inatafutwa kwa gharama, najua waandamanaji watakaokuwa mstari wa mbele watapigwa risasi. Nasema hivyo hivyo ili muwe tayari kwa lolote lile,” amesema Mbowe.
Chanzo: habari5

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top