
Wafungwa wawili wamepigwa risasi na kufa wakati wakijaribu kutoroka katika mahakama moja nchini Afrika Kusini, mamlaka zinasema.
Afisa kutoka wizara ya sheria ameliambia shirika la habari la Afrika Kusini -SAPA- kuwa wafungwa hao waliokuwa wakisubiri kesi yao kusikilizwa, walichukua bunduki iliyokuwa imefichwa kwenye pipa la taka.
Kulikuwa na kurushiana risasi na maafisa wa polisi.
Tukio hilo limetokea katika mahakama kuu ya Mthatha iliyopo katika jimbo la Eastern Cape. BONYEZA HAPA
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment