Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Nyuki bana, nao wana yao. Katika mechi ya Ligi Kuu Bara, Jumapili iliyopita wakati Mtibwa Sugar ikiivaa Yanga, waliwakimbiza wachezaji wa Mtibwa. Wachezaji hao walikuwa wanashangilia bao lililofungwa na mwenzao Mussa Hassan Mgosi, ghafla nyuki hao wakaibuka na wachezaji hao wakalazimika kutimua mbio.
Cameraman wa Azam FC na mwenzake, pia walilazimika kuacha kazi yao na kutimua mbio baada ya lundo hilo la nyuki kuungana nao wakati wakishangilia. Hata hivyo halikuwa tukio la muda mrefu, nyuki hao ‘walichukua za time’. Mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara iliisha kwa Mtibwa Sugar kushinda kwa mabao 2-0 kwenye uwanja wa Jamhuri.
Picha na salehjembe

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top