Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


http://a.files.bbci.co.uk/worldservice/live/assets/images/2014/07/26/140726162438_tripoli_airport_road_fighting_304x171_reuters.jpg 
http://a.files.bbci.co.uk/worldservice/live/assets/images/2014/07/15/140715040948_tripoli_airport_512x288_afp_nocredit.jpg                          Uwanja wa ndege wa Tripoli
Muungano mmoja wa wanamgambo nchini Libya unasema kuwa umeuteka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Tripoli baada ya mapigano makali kati yake na kundi pinzani la waasi
Picha zilizowekwa katika mtandao zimeonyesha wapiganaji hao wakisherehekea juu ya ndege na katika majengo ya uwanja huo.
Muungano huo unaoshirikisha wanamgambo wa kiislamu pamoja na wanamgambo kutoka mji wa Misrata umesema kuwa uliuteka uwanja huo licha ya mashambulizi ya angani yanayodaiwa kutekelezwa na Misri pamoja na nchi za ufalme wa kiarabu.
Mwandishi wa BBC mjini Tripoli anasema kuwa kuna ripoti za kuendelea kwa vita kati ya makundi pinzani viungani mwa mji huo.
Uwanja huo umefungwa kwa takriban mwezi mmoja sasa kufuatia vita kati ya makundi pinzani ya wanamgambo yaliozuka tangu kuondolewa madarakani kwa aliyekuwa rais wa taifa hilo kanali Gaddafi mwaka 2011.
Bonyeza Hapa


Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top