




Na.Festo Sanga.
Naibu waziri wa Fedha na Naibu Katibu Mkuu wa
CCM Tanzania Bara Mh:Mwigulu Nchemba jana alifanya jambo kubwa na lakibinadamu kwa kuamua kusitisha safari yake kwa muda akielekea Iringa iliasaidi Majeruhi wa ajali ya Roli Kubwa lililokuwa likitokea Dsm kuelekea Barabara ya Iringa.
Ajali hiyo ambayo ilitokea mbele ya Mh:Mwigulu Nchemba aliyekuwa nyuma ya Roli hilo kabla ya Kugonga Ukuta na Kuanguka haikuleta madhara makubwa.
Mh:Mwigulu Nchemba ambaye ni mara kadhaa amekuwa akisaidia kuokoa majeruhi kwenye ajali anapokutana nazo barabarani,hata kwenye ajali hii alilazimika kuhakikisha majeruhi wanaokolewa na kukimbizwa Hospitali kabla ya hatua kubwa zaidi za Hospitali kuendelea,Katika ajali hiyo Mh:Mwigulu Nchemba alitumia Boksi lake la Msalaba Mwekundu(First Aid Kit) kuhudumia majeruhi hao iliwasitoke sana Damu.
Wananchi na Madreva waliopata kusimama kwenye ajali hiyo,Walimpongea sana Mh:Mwigulu Nchemba kwa namna alivyosaidia kuokoa Watanzania wenzake kwenye ajali hiyo,Wengi walisikika wakiomba Viongozi wengine waige mifano hii ya Mwigulu ya Kusimama na kuhudumia wahanga wa ajali,Kwa sababu imekuwa ikitokea Viongozi wanapoona ajali hawasimami kwa madai wanawahi ratiba za kazi zao.
Bonyeza Hapa
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment