
UMOJA wa
Katiba ya Wananchi (Ukawa), umemtaka Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto
Kabwe (Chadema), kuacha kuwaingilia kwenye mambo kwa vile
hayamhusu.Kauli ya Ukawa imekuja siku moja baada ya Zitto kusema hana
uhakika na wala haamini kama umoja huo utakuwa endelevu hadi uchaguzi
mkuu mwaka 2015, kwa sababu si mara ya kwanza vyama vya upinzani
kuungana kisha kugawanyika.Alisema siku zote Watanzania wanapenda kuwa
na upinzani imara ambao watu wanaweka maslahi yao pembeni na kuungana
dhidi ya chama kilichopo madarakani.Akizungumza na MTANZANIA mjini Dar
es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), Dk. Willibrod Slaa, alisema haoni umuhimu wa kujibizana na
mtu aliye nje ya umoja huo kwa sababu hawezi kujua dhumuni la kuungana.
“Hatuhitaji
kuumiza kichwa wala kujibizana na mtu aliye nje ya Ukawa, kwa sababu
hajui ulianzishwa kwa lengo gani, atabaki kutabiri kitu ambacho hana
uhakika nacho, bali anazungumza kutokana na matakwa yake.
“Kwanza
si msemaji wa Ukawa, tunashangaa hata kukaa na kuanza kujadili suala
lisilomhusu, ni nani na ninyi waandishi wa habari mnapaswa kumuuliza
maswali wakati akizungumza hayo,” alisema Dk. Slaa.
Alisema
Ukawa haufanyi kazi kwa kufuata maneno ya barabarani, bali wanafanya
kazi kwa vitendo, ikiwa ni pamoja na kusikiliza maoni ya wananchi nini
wanataka ili waweze kuyafanyia kazi.
Alisema
tangu kuanzishwa kwa umoja huo, wamekwenda zaidi ya mikoa 17 na majimbo
yake ili kusikiliza maoni ya wananchi ambayo wameyachukua na kuyafanyia
kazi, hivyo basi hawana muda wa kukaa na kujadili kauli za watu
zinazotolewa barabarani za kujadili masuala yasiyowahusu.
“Sisi
tunafanya kazi na Watanzania, hatufanyi kazi na mtu mmoja mmoja, ndiyo
maana tulikwenda mikoa 17 na majimbo yake kwa ajili ya kuwaelezea umoja
wetu na mikakati tuliyopanga ndani ya umoja huu, hivyo basi hatuna
nafasi ya kujadili kauli ya mmoja mmoja,” alisema.
Alisema
kutokana na hali hiyo, viongozi wa umoja huo hawawezi kuishi kwa imani,
bali wanafanya kazi kwa vitendo ili wananchi waweze kuwahukumu katika
uchaguzi ujao.
Alisema
Ukawa haupo kwa ajili ya Katiba peke yake, bali ni kuangalia maslahi ya
wananchi katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii ili kuhakikisha
wanaondokana na hali ngumu ya maisha na kupata mafanikio.
Alisema
mkakati uliopo ni kuhakikisha malengo hayo yanatekelezwa kwa vitendo ili
wananchi wenyewe waweze kuwanyooshea vidole kwenye chaguzi zijazo.
Naye
Katibu wa Ukawa ndani ya Bunge, Julius Mtatiro, alisema mawazo ya mtu
yanapaswa kuheshimiwa, lakini umoja huo hauwezi kufanya kazi ya utabiri
kama utaendelea au kuvunjika.
“Ukawa
hauwezi kufanya kazi ya utabiri, kwa sababu tulipoungana tulikuwa na
malengo ya dhati, ikiwa ni pamoja na kuondoa tofauti zetu na kuangalia
maslahi ya wananchi na si kauli ya mmoja mmoja, japo naheshimu mawazo
yake,” alisema Mtatiro.
Mtatiro
alitolea mfano kwa kusema kauli ya Zitto ni sawa na falsafa ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM), ambayo wamekuwa wakitangaza kila kona kuwa upinzani
Tanzania unaelekea kufa wakati si kweli.
WAJUMBE
Katika
hatua nyingine, Ofisi ya Katibu wa Bunge Maalumu la Katiba imewataka
wajumbe wa Bunge hilo kuwasili Dodoma Agosti kwa ajili ya kuanza mkutano
huo kama ulivyopangwa.
Taarifa
iliyotolewa kwa vyombo vya habari mjini Dar es Salaam na ofisi hiyo,
ilisema Bunge Maalumu la Katiba linatarajia kuanza vikao vyake Agosti 5,
mwaka huu mjini Dodoma.
Taarifa
hiyo ilisema Agosti 4 itakuwa siku maalumu kwa ajili ya mambo ya
kiutawala, hivyo wajumbe wote wanapaswa kufika Ofisi za Bunge Dodoma
kuanzia saa 4:00 asubuhi.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyza hapa
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment