Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu akiwa na mama yake.
Na Waandishi Wetu
STAA wa filamu Bongo, Wema Sepetu ametaja sababu zinazomfanya aingie katika mgogoro na mama yake mzazi, Miriam Sepetu kuwa ni suala la uchumba wake na Nasibu Abdul ‘Diamond’ ambao alikuwa akiupinga mara kwa mara.
Staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu.
Akipiga stori na mapaparazi, Wema alisema kwa muda mrefu alikuwa akitofautiana kauli na mama yake katika suala zima la uhusiano wake na Diamond lakini anamshukuru Mungu amemuelewa na sasa kila kitu kinakwenda sawa.
“Mama nilikuwa nikimsihi sana juu ya uchumba wangu na Diamond lakini sasa tumefikia hatua nzuri namshukuru Mungu amekubali, maana siku hizi nikionana naye ananiuliza vipi mwenzako mzima, anaendeleaje, wakati mwanzoni haikuwa hivyo,” alisema Wema huku akiahidi kumkutanisha Diamond na mama yake. Imeandikwa na Mayasa Mariwata na Shani Ramadhani.
KIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331

kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyza hapa
 

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top