Msichana wa kazi za ndani, Fonolia Lembres (12) aliyeshambuliwa kwa mapanga na tajiri wake, Emmanuel Msovera.
Msichana
wa kazi za ndani, Fonolia Lembres (12) amenusurika kuuawa na mwajiri
wake aliyetambulika kwa jina la Emmanuel Msovera ambaye ni kondakta wa
Hiace, baada ya kushambuliwa kwa kipigo na kukatwakatwa mapanga
mwilini.Fonolia ambaye kwa sasa amelazwa katika Hospitali ya Mkoa
Mount-Meru, jijini hapa, amejeruhiwa vibaya kwa kukatwa kiganja cha
mkono wa kushoto na maeneo mengine ya mwili kisa kikidaiwa kuwa ni
kutuhumiwa kuiba shilingi 30,000 za bosi wake huyo.
Hata
hivyo, majirani na nyumbani kwa mtuhumiwa huyo wameeleza kuwa msichana
huyo amekuwa akipigwa kama mbwa mwitu kila siku kiasi cha wao kumtaka
mtuhumiwa amrejeshe kwao iwapo ameshindwa kukaa naye.
Akizungumza
kwa tabu akiwa hospitali alikolazwa , mfanyakazi huyo wa ndani
alilalamika kutoona vizuri kutokana na jicho lake la kushoto kupigwa
ngumi pia maumivu makali ya mkono pamoja na sehemu zingine alizokatwa
kwa panga na fyekeo.
Akisimulia
tukio hilo alisema, mke wa mtuhumiwa, Rose Benjamini, mumewe
alimchukuwa binti huyo kwa wazazi wake miaka minne iliyopita kwa
makubalino ya kumsomesha lakini badala yake akawa anampiga mara kwa
mara.
Alisema
maisha yake yote yamekuwa ya mateso makubwa kwani amekuwa akipigwa na
kunyanyaswa kwa kiwango kikubwa na wakati mwingine hata kunyimwa chakula
ambapo alikuwa akivumilia mateso hayo.
Alisema
siku ya tukio (Jumamosi iliyopita) usiku majira ya saa tatu, Benjamini
ambaye ni kondakta wa Hiace zinazofanyakazi kati ya mjini na kwa
Morombo, alifika na kumuuliza kuhusu fedha zake kiasi cha shilingi elfu
30 alizoziacha kwenye kochi.
“Nilimwambia
sikuchukua ndipo alichukuwa panga na kunikata mkono, baadaye alichukuwa
fyekeo na kunikata mguuni na sehemu zingine na kunipiga ngumi kwenye
jicho,’’ alisema mwanafunzi huyo.
Baadhi
ya majirani walioshuhudia tukio hilo walitoa taarifa kwa balozi wa eneo
hilo, Joseph Mtinangi ambaye alichukuwa jukumu la kutoa taarifa polisi
ambao walifika na kumkuta mtuhumiwa amejifisha
juu ya dari katika chumba chake, wakamkamata na kumfikisha kituo kikuu cha polisi jijini hapa.
Mtuhumiwa
huyo amefunguliwa hati ya mashitaka yenye kumbukumbu namba
AR/RB/10071/2014 KUJERUHI.Kwa upande wake balozi Mtinangi alilaani tukio
hilo na kueleza kuwa ni tukio la kinyama ambalo mtuhumiwa amekuwa
akimtendea mara kwa mara msichana huyo.
Aliongeza
kuwa alikuwa akipata malalamiko juu ya tukio hilo ambapo aliwaonya
wahusika lakini kwa kitendo alichokifanya siku hiyo ametoa wito kwa
vyombo vya dola kuchukuwa hatua kali ili iwe fundisho kwa wengine wenye
tabia kama hiyo.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyza hapa
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment