
Shirika
la kutetea haki za wanyama la Afrika Kusini limeanza uchunguzi
kuhusiana na kifo cha twiga baada ya kuumia wakati akisafirishwa kwenye
gari. Watu walioshuhudia tukio hilo wanasema twiga mmoja kati ya wawili
waliokuwa kwenye lori, aligonga kichwa chake katika barabara moja mjini
Johannesburg. Gari hilo baadaye liliharibika na kulazimika kusubiri kwa
saakadhaa kabla ya kutengenezwa.
Wanyama
wote wawili walipelekwa kwa daktari wa wanyama, lakini shirika la
kutetea haki za wanyama la NSPCA limesema twiga mmoja alikufa. Tukio
hilo limeleta mjadala mkubwa kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter.
Meneja wa NSCPA Rick Allen amethibitisha kuwa twiga huyo alipata
majeraha ya kichwani lakini amesema uchunguzi ni muhimu ufanyike
kutafuta sababu hasa ya kifo hicho.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyza hapa
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment