Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

SHIRIKA la Ugavi wa Umeme (Tanesco) Mkoa Pwani, limefanikiwa kumkamata Jeams Mkelembwa ambaye anadaiwa kuwatapeli wananchi kwa kujifanya mtumishi wa shirika hilo.
Akizungumza kuhusu sakata hilo jana, Ofisa Usalama wa Tanesco Pwani, Henry Byarugaba, alisema kwamba tukio la kukamatwa kwa mtuhumiwa  huyo lilitokea juzi wilayani Kisarawe wakati alipokuwa akitaka kumtapeli mteja mmoja  wa umeme.
Byarugaba alisema mtuhumiwa huyo amekuwa akitumia njia mbalimbali ikiwemo kutumia majina ya viongozi, pamoja na kudai yeye ndiye Meneja wa Tanesco Mkoa wa Pwani, kitu ambacho si cha kweli.
 
“Ndugu mwandishi, katika siku za hivi karibuni tulikuwa na zoezi maalumu la kukagua miundombinu yetu ya umeme katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Pwani, lakini tulipata fununu kuna baadhi ya watu wanajifanya wao ni wafanyakazi wa shirika letu na kuwatapeli wateja wetu, hali ambayo inasababisha lawama nyingi kutolewa kwetu…

“Huyu jamaa tuliyemkamata ni hatari sana, kwani ameshafanya matukio mengi ya utapeli kwa wananchi, maana anatumia vyeo vya watu mbalimbali ikiwemo kujifanya yeye ni ofisa wa Tanesco, mara mtumishi kutoka wizara fulani mara Takukuru, yaani ni balaa tupu, kumbe ni kishoka maarufu sana na mimi nitahakikisha anachukuliwa hatua kali za kisheria ili iwe fundisho,” alisema Byarugaba.

Alisema mtuhumiwa huyo kwa sasa anashikiliwa na polisi Kisarawe na kuwaomba wateja wote ambao wametapeliwa na mtu huyo waende kwa ajili ya kumtambua.

Byarugaba aliongeza kuwa tapeli huyo alishafanya matukio ya kuwaibia watu katika maeneo mbalimbali ikiwemo Majohe, Pugu, Chanika na mengineyo.
 
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331

kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyza hapa

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top