Kuna
kipindi stori za namba ambazo wengi walikua wakisema za ajabu na endapo
zikikupigia usipokee zilikuwa zikitawala sana kwenye mitandao ya
kijamii na wengi pia walikua wakizonyesha namba hizo.
Tunda Man ambaye pia ni miongoni mwa watu wanaounda kundi la Tip Top
Connection Jioni ya July 28 amepata simu hiyo ambayo amedai kwake ilikua
ni mara ya kwanza kupigiwa kwani namba hizo hajawahi kuziona zikimpigia
kabla.
’Nilikua nafuturu jana jioni wakati naendelea kufuturu nikapigiwa simu
namba sikua nazijua kwani zilikua za maajabu tu,sikupokea,ilipiga kama
mara 30 hivi’
‘Baadae nikapokea na kisha nikaiweka mbali kidogo na mimi wakati nasema
hallow ghafla kitu kama shoti ya umeme kikaanza kutembea kwenye viganja
mpaka kwenye mkono nikakosa nguvu kabisa nikawaambia jamani nipelekeni
hospital’
‘Tukaenda hospital ya Serikali hapo Palestina,Dokta akasema huu ugonjwa
tangu ameanza kutibia watu hajakutana nao ni mara yake ya kwanza hivyo
matibabu aliyokuwa akinipatia ni kama ya mtu aliyepooza ghafla’
‘Kwa sasa namshukuru Mungu naendelea vizuri ingawa kuna dawa nimepewa
zingine nameza mara 2 kwa siku na vidonge vingine ni mara 3 kwa siku pia
nimechomwa sindano’
Hii ndiyo namba iliyompigia Tunda

UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyza hapa
Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi
Post a Comment
Post a Comment