Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Deogratius liyunga akiwa hodini
WATU wasiofahamika wamemvamia makamu Mwenyekiti wa uwenezi kanda ya Magharibi chama cha Democrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Kigoma Deogratius Liyunga mkazi wa Mwanga Kusini Manispaa ya Kigoma Ujiji na  kumjeruhiwa maeneo mbalimbali ya mwili wake ambapo amelazwa katika hospitali ya Rufaa Maweni Mkoani humo..
Akizungumza hilo kiongozi huyo alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 4:00 usiku akiwa anatoka maeneo ya Mwanga katika eneo la Urusi ambapo alikuwa akiangalia mpira kuelekea nyumbani kwake.


Alisema kuwa akiwa njiani alikutana na watu wanane ambapo mtu mmoja alimkaba shingoni na mwengine kumpiga na ubao maeneo ya mgongoni huku mwingine akitumia kisu kutaka kumchoma ndipo alikishika kisu hicho na kumuachia majeraha maeneo ya mkononi.

Alidai  kuwa watu hao waliomshambulia usiku huo wanasadikiwa kuwa ni wafuasi wa chama cha siasa cha Alliance for Change and Transparence (ACT) ambacho kimeanza hivi karibuni mkoani humo ambapo walichukua kiasi cha shilingi 63,000.
Alisema awali watu hao walimpatia vitisho vya hapa na pale ambapo matukio hayo ya vitisho yamekuwa yakijitokeza kwa viongozi wa chama cha Chadema Mkoa wa Kigoma hivyo tukio hilo kuhusishwa na harakati za kisiasa.


“Hali ya afya bado si nzuri nahisi maumivu makali katika  maeneo mbalimbali ya mwili na mkono bado unamaumivu makali hivyo naendelea kupata matibabu  na viongozi wa chama wanakuja kuniangalia ambao wamenipa msaada mkubwa wa kunifikisha hospitali”alisema Liyunga.


Akizungumzia tukio hilo katibu wa chama hicho wilaya ya Uvinza Shabani Madede amesema alipatiwa taarifa hiyo majira ya saa nane usiku ambapo awali walikuwa na kiongozi huyo wakiangalia mpira wa kombe la dunia unaendelea nchini, ambapo walikuwa maeneo ya Urusi na kudai kuwa majira ya saa mbili waliondoka na kumuacha akiendelea kuangalia mpira huo.

Kamanda wa polisi mkoa Frasser Kashai alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo kutokea katika manispaa ya Kigoma Ujiji Mkoani humo hakuwa na taarifa ya tukio hilo na kuahidi kufanya ufuataliaji. 
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top