MKONGWE wa Bongo Fleva, Godfrey Tumaini ‘Dudubaya’
anasakwa na polisi kwa RB namba OB/RB/11650/2014 KUTISHIA KUUA mganga wa
jadi Mery Kapalisya ambaye inadaiwa alikuwa akiishi naye kama mkewe.
“Mimi na Dudu (Dudubaya) tulikutana baada ya kukutanishwa na Mabovu
(msanii) ndipo tukaanzisha uhusiano wa kimapenzi baada ya kuniomba niwe
naye na kunieleza matatizo yake.
“Kwa sababu nilimpenda niliamua kumkubalia na kuanza naye maisha ambapo tulikuwa tukilala katika baa yangu nyumbani kwa akina Mabovu.
“Tukiwa ndani ya uhusiano, Dudubaya alianza kunibembeleza kwamba baa ile tuipe jina la Mamba ikiwa ni chata yake, kwa sababu nilimpenda niliamua kumkubalia lakini nilimwambia aongeze herufi nyingine mbili ambazo zitamaanisha na mimi nahusika, tukakubaliana,” alisema Mery na kuongeza:
“Baada ya baa kubadilishwa jina, matatizo yakaanza taratibu kwani walijaa wasanii wa kila aina, baa ikaanza kuwa na sifa mbaya mpaka wateja wote wakaondoka wale waliokuwa wanajiheshimu.”
Mery alisema alikuwa akimuonya Dudubaya juu ya tabia za kumsaliti na kulala na wanawake ndani ya nyumba pale anapokuwa amesafiri kwenda kwenye mambo ya kitabibu lakini alikuwa hasikii.
“Baada ya kunifukuza nyumbani, amenitumia maneno mazito sana ambayo siwezi kusimulia kiukweli lakini ninao ushahidi wa SMS,” alisema Mery alipokuwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay.
Wakati Mery alipokuwa kituoni hapo, polisi walimpigia simu Dudubaya, akasikiliza maelezo ya polisi kisha akakata simu na alipopigiwa tena, hakupokea. Bonyeza hapa kuangalia mahojiano
Akisimulia mkasa mzima, Mery alisema
Dudubaya alitishia kumuua mara baada ya kumfukuza katika nyumba
waliyokuwa wakiishi pamoja maeneo ya Tandale, jijini Dar.
“Kwa sababu nilimpenda niliamua kumkubalia na kuanza naye maisha ambapo tulikuwa tukilala katika baa yangu nyumbani kwa akina Mabovu.
“Tukiwa ndani ya uhusiano, Dudubaya alianza kunibembeleza kwamba baa ile tuipe jina la Mamba ikiwa ni chata yake, kwa sababu nilimpenda niliamua kumkubalia lakini nilimwambia aongeze herufi nyingine mbili ambazo zitamaanisha na mimi nahusika, tukakubaliana,” alisema Mery na kuongeza:
“Baada ya baa kubadilishwa jina, matatizo yakaanza taratibu kwani walijaa wasanii wa kila aina, baa ikaanza kuwa na sifa mbaya mpaka wateja wote wakaondoka wale waliokuwa wanajiheshimu.”
Mery alisema alikuwa akimuonya Dudubaya juu ya tabia za kumsaliti na kulala na wanawake ndani ya nyumba pale anapokuwa amesafiri kwenda kwenye mambo ya kitabibu lakini alikuwa hasikii.
“Baada ya kunifukuza nyumbani, amenitumia maneno mazito sana ambayo siwezi kusimulia kiukweli lakini ninao ushahidi wa SMS,” alisema Mery alipokuwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay.
Wakati Mery alipokuwa kituoni hapo, polisi walimpigia simu Dudubaya, akasikiliza maelezo ya polisi kisha akakata simu na alipopigiwa tena, hakupokea. Bonyeza hapa kuangalia mahojiano
>Credit GPL
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment