Mahakama ya
Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro imewabadilishia mashtaka washitakiwa
watatu katika kesi ya marehemu, Nasra Mvungi (4) waliokuwa wanakabiliwa
na makosa ya kula njama na kufanya ukatili, sasa wanashitakiwa kwa kosa
la kusababisha kifo cha mtoto huyo.Watuhumiwa waliofikishwa, mahakamani
hapo jana ni pamoja na baba mzazi wa Nasra, Rashid Mvungi (47), mkazi wa
Lukobe na mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro pamoja na
wanandoa Mariam Said (38) na mumewe Mtonga Omar (30), wakazi wa Mtaa wa
Azimio, Kata ya Kiwanja cha Ndege.Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa
wa Morogoro, Mary Moyo, Mwendesha Mashitaka na Wakili wa Serikali,
Sunday Hyera, kwa kushirikiana na wenzake, Wakili wa Serikali, Edgar
Bantulaki na Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Zabron Msusi, waliiomba
Mahakama hiyo kuwasomea shitaka jipya la mauaji chini ya kifungu namba
196 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai na kwamba shitaka hilo
halitawaruhusu washitakiwa kujibu lolote.
Alidai
mahakamani hapo kuwa katika tarehe tofauti ya mwezi wa Desemba mwaka
2010 hadi mei 2014 katika maeneo ya Kiwanja cha Ndege washitakiwa hao
kwa nia ovu walimtesa mtoto Nasra Mvungi na kumsababishia kifo chake
Juni Mosi mwaka huu.
Hata
hivyo, Hakimu Moyo alisema kwa mujibu wa sheria, Mahakama hiyo haina
mamlaka ya kusikiliza shitaka hilo na hivyo kuiahirisha hadi Juni 26,
mwaka huu itakapofikishwa mahakamani hapo kwa kutajwa tena.
Watuhumiwa wote watatu walirudishwa rumande kwa kuwa shitaka hilo halina dhamana.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment