Wapiganaji wa Jihadi wameendelea
kuyateka maeneo zaidi nchini Iraq,baada ya kuliteka eneo moja la kivuko
karibu na mpaka wa Syria, na sasa wanalekea mjini Baghdad kupitia bonde
la Euphrates.
Mwandishi wa BBC nchini Iraq amesema kuwa hatua hiyo inawafungulia njia wapiganaji wengine wa ISIS nchini Syria.
Wapiganaji hao vilevile wameiteka miji zaidi
katika mkoa wa Anbar ambapo mwandishi huyo anasema kuwa lengo lao ni
kuitumia kuvamia mji mkuu wa Baghdad.
Wanamgambo wa Kishia hapo jana walifanya gwaride mjini Baghdad, na kuzua wasiwasi kuhusu tofauti inayozidi kuibuka kati ya watu wa dhehebu la kishia na wale wa Kisunni.
BONYEZA HAPA
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment