Serikali ya Kenya imewataka wananchi kuangalia mechi za michuano ya
kombe la dunia katika maeneo ya majumbani badala ya sehemu za wazi
zilizojazana na ambazo hakuna ulinzi.
Ushauri huo umetolewa kufuatia siku mbili za mashambulizi katika mji wa Pwani wa nchi hiyo na kusababisha vifo vya watu 60.
Mashambulizi hayo yalianzia katika eneo la Mpeketoni ambako mashabiki walikuwa wakiangalia mpira siku ya Jumapili.
Waziri wa usalama wa ndani amesema licha ya kuwa ulinzi umeimarishwa
katika maeneo mbalimbali nchini, wamiliki wa baa na migahawa wanatakiwa
kuchukua tahadhari zaidi.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment