Meneja
wa Jahazi Modern Taarab, Mohammed Rashid Mauji 'Father Mauji' pamoja na
shabiki wa Jahazi wakizindua albamu mpya iitwayo Chozi la Mama.
Mwimbaji
nyota wa muziki wa taarab nchini, Mzee Yusuf (kulia) akiongea jambo
kabla ya uzinduzi wa Chozi la Mama. Katikati ni Aisha Abushily 'Mama wa
madikodiko' kutoka Pilipili FM ya Kenya.
Mzee Yusuf akiimba wimbo wa Chozi la Mama uliobeba jina la albamu iliyozinduliwa usiku huu Dar Live.
MC
wa leo katika uzinduzi wa albamu mpya ya Jahazi, Aisha Abushily 'Mama
wa madikodiko' (kushoto) akiwa katika pozi na Leila Salim 'Aunt Liloo'
wote kutoka Mombasa, Kenya.
Wadau wa Jahazi, Injinia Arnold Gabone (kushoto) na mwenzake wakiwa katika pozi wakati wa uzinduzi wa Chozi la Mama.
Jahazi Modern Taarab chini ya kiongozi wake Mzee Yusuf
'Mfalme' imezindua albamu mpya iitwayo Chozi la Mama yenye jumla ya
nyimbo sita usiku huu ndani ya Ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala Zakheem
jijini Dar. Albamu hiyo ni ya 10 tangu kuanzishwa kwa kundi hilo.
(PICHA: GABRIEL NG'OSHA NA DENNIS MTIMA / GPL)
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment