Kijana
mmoja mkazi wa kijiji cha Nyambogo wilayani Rorya mkoani Mara, ambaye
anadaiwa kupotea nyumbani kwa imani za kishirikina hatimaye amepatikana
huku akiwa katika hali ya kutisha bila kujitambua na mwili wake ukiwa
umejaa tope jingi, tukio ambalo limevuta mamia ya wananchi wa kijiji
hicho.
kijana
huyo Kenedy oguko mwenye umri wa miaka 22 amekutwa nje ya nyumba yao
asubuhi ya Juni tano mwaka huku,akiwa uchi wa mnyama,ambapo baadhi ya
mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa tangu kutoweka kwa kijana huyo
siku nne zilizopita,wamekuwa wakimtafuta bila mafanikio huku wakihusisha
tukio hilo limefanywa kwa imani za kishirikina.
kwa
upande wake mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Rorya Bw Samwel
Kiboye,ambaye ni miongoni mwa mashuhuda wa tukio hilo,amewaomba wananchi
kuacha kulipiza visasi kwa kuwasaka watu wanaotuhumiwa kwa ushirikina
bali watumie vyombo vya dola huku mwenyekiti wa kijiji hicho akilaani
vikali vitendo hivyo vya ushirikina vinavyoendelea kijijini hapo hatua
ambayo amesema imesabisha wananchi sasa kuishi kwa hofu kubwa.
hata
hivyo katika hali ya kushangaza wazee wa jadi kijijini hapo waliagiza
kila mwananchi kupita mbele ya kijana huyo na kumpa mkono kama njia moja
wapo ya kuwezesha kupata fahamu kitendo ambacho hata hivyo hakikuzaa
matunda.
ANGALIA VIDEO HAPA CHINI
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment