Hatua
hiyo ni ya kuchunguza madai ya kuvaa sketi fupi ambayo imesemwa kuwa
ilikua nje ya maadili ya kazi na sheria za Jeshi hilo la Polisi la
nchini Kenya.
Kupitia
kwa wakili wake Tom ojienda Koplo Lindah amesema kwamba hakufanya kosa
lolote kuvaa sketi hiyo hadi kulazimika kuundwa kamati ya kumchunguza na
kutoa maelekezo ya adhabu anayostahili.
Lindah
amesema kwamba asubuhi ya April 26 alifanya mkutana na OCPD wa kituo
cha kiambu ili kuelekezwa,ingawa mkuu huyo wa polisi hakusema lolote
kuhusiana na mavazi aliyovaa.
Ingawa
May 2 Lindah alichukuliwa hatua za kinidhamukwa kosa la kuvaa mavazi
yaliyombana kulingana na sheria za huduma za polisi-alivyo kuwa amevalia
sketi fupi iliyombana saa saba mchana nje ya tawi la benki ya KCB
lililopo kiambu.
Linda
amedai kwamba sketi iliyo zua utata alikabidhiwa na afisa anaye
shughulika na sare za polisi mwaka 2003 na amekua akivaa kila siku na
mabosi wake hawakuwahi kulalamika kabla ya tarehe 26 Aprili.
Wakili
wake Ojienda amesema kwamba wakati wa kikao cha kamati hiyo may 7 na
may 9 Bii Okelo alichukuliwa hatua kimakosa kwani hakukua na sababu za
kumuhukumu kulingana na mavazi yake,kesi yake itatajwa june 12 mwaka
huu.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment