Sina uhakika kama mapenzi ni machaguo au ni zali na hayana formula,
of course mimi sio mtaalam wa saikolojia na mahusiano. Ila naamini kati
ya hayo kuna jibu.
Muigizaji wa kike mwenye umbo matata na sura yenye mvuto, Irine Uwoya
ana machaguo yake na ameweka wazi sifa za mwanaume ambaye anaweza
kumvutia/kutamani kuwa nae.
“Awe kijana mzuri asiye na kitambi.” Uwoya ameliambia jarida la VibeTz lililotoka leo.
Hata hivyo, mrembo huyo mtoto mmoja ameshanyakuliwa na Msami ndio mwenye bahati.
Uwoya hakusita kujivunia mkwanja alionao. Aliambiwa kuchagua kwa sasa
kati ya umaarufu na mtonyo alichagua umaarufu na kueleza kuwa ‘mtonyo
anao mwingi tu’.
Post a Comment
Post a Comment