Kilichowakera
abiria ni kupewa taarifa hiyo ghafla tena bila kuelezwa sababu ya hatua
hiyo. Mzozo huo ulizimwa kwa busara za askari polisi wa reli na wa
kampuni binafsi ya ulinzi waliokuwapo katika stesheni hiyo
Kampuni
ya Reli Tanzania (TRL), imesitisha safari za treni ya Reli ya kati kwa
siku saba kutokana na kubainika hitilafu katika Daraja la Ruvu.
Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni hiyo, Kipallo Kisamfu alisema: “Itachukua takriban
siku saba hivi hivyo kuanzia jana (juzi), eneo la reli lenye urefu wa
kilometa 82 kutoka Dar es Salaam hadi Ruvu limesitishwa kwa muda kutoa
huduma ya usafiri wa reli.”
Juzi,
shirika hilo lilitangaza kusitishwa ghafla kwa safari kutokana na
kubainika kuwepo nyufa katika daraja hilo na kuzua vurumai baina ya
maofisa wa TRL na abiria.
Kilichowakera
abiria ni kupewa taarifa hiyo ghafla tena bila kuelezwa sababu ya hatua
hiyo. Mzozo huo ulizimwa kwa busara za askari polisi wa reli na wa
kampuni binafsi ya ulinzi waliokuwapo katika stesheni hiyo.
Ofisa
Habari wa TRL, Midradjy Maez alisema baadaye kuwa usafiri huo
umesitishwa kutokana na kubainika kwa nyufa hizo na timu ya wahandisi wa
kampuni hiyo ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji ilikuwa imekwenda eneo
la tukio.
Chanzo:Mwananchi
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment